Hata hivyo, nawashukuru sana wasomaji wangu kwa mada ile kwani nilipokea simu nyingi za kunipongeza kwamba nilichokiandika kilikuwa cha kweli tupu.
Mada ya leo ni; Je, Usingefanyiwa Kitchen Party? Imezoeleka kwamba, katika miaka ya kimaendeleo wanawake wamekuwa wakipitia hatua kuu mbili mpaka kufikia ndoa ambayo ni hatua ya tatu.
KITCHEN PARTY
Hii ni hatua ya kwanza baada ya mwanamke kuchumbiwa na kulipiwa mahari. Kitchen Party ni tukio la bi harusi mtarajiwa kuchota mafunzo mbalimbali kuhusu maisha atakayokwenda kuishi ndani ya ndoa.
Kwa kawaida, siku ya Kitchen Party, bi harusi hupewa somo na waalikwa kwenye sherehe hiyo, hawa watu wazima waliomo kwenye ndoa tayari wakimwambia jinsi ya kuishi na mumewe katika maisha ya ndoa.
“Ukifika kwa mumeo, mheshimu. Jua yeye ndiye mume. Siyo unafika kwa mume wewe unaanza kujifanya kidume. Unashindana naye. Akikukwaza kidogo tu, wewe unasema mpaka majirani wanasikia. Utaachika!
“Mume anataka matunzo. Siyo unafika kwa mumeo, anatoka asubuhi shati chafu, mkanda wa suruali umeruka luksi mbili, soksi amerudia za wiki jana. Hapo utakuwa huna sifa ya kuwa mke,” maneno hayo niliwahi kuyasikia kwenye mkanda mmoja wa video uliorekodiwa kwenye Kitchen Party iliyofanyika kwenye ukumbi, Sinza-Mori, Dar es Salaam.
SEND OFF
Hii ni sherehe ya pili na ya mwisho kabla bi harusi hajaingia kwenye ndoa. Send Off hufanywa na wazazi wa bi harusi mtarajiwa. Sherehe hii ni ya wazazi wanamuaga binti yao na kumtakia heri kwenye maisha ya ndoa.
Mara nyingi Kitchen Party, Send Off na ndoa hupishana siku chache. Wengine hata ndani ya wiki moja mambo yote matatu hufanyika!
CHA AJABU SASA
Kinachoshangaza sasa pamoja na mafunzo ya Kitchen Party, ndoa za siku hizi zinaonekana ndizo zenye wanawake wenye upinzani mkubwa ndani ya nyumba, baadhi yao wakitaka kuoneshana ubabe na waume zao.
Baadhi ya wanawake (nasisitiza baadhi) walio ndani ya ndoa siku hizi wana tabia ya kutopika chakula kwa sababu ya kuogopa kuharibu rangi za kwenye kucha. Kazi ya kupika kwa sasa inamhusu zaidi msaidizi wa kazi za ndani ‘hausigeli’.
Hawa wasaidizi wa kazi za ndani wamekuwa ndiyo wenye majukumu makubwa ya wamama wa familia na mabosi wao wa kike ndiyo wamekuwa wasaidizi wa kazi za ndani! Si sawasawa!
MZOZO NDANI
Imefika mahali, ndani ya ndoa kila mmoja (mume, mke) anataka kuwa na sauti kuliko mwenzake na kusababisha majirani kushindwa kujua nani mke nani mume ndani ya nyumba. Lakini ikumbukwe kwamba mwanamke huyo ametoka kupewa semina ya kuishi ndani ya ndoa.
Wako wanaume wanaolalamika kwamba, wake zao ni ‘milopolopo’, yaani wana midomo. kupitiliza. Akianza kupayuka kwa jambo f’lani ni kama cherehani na ndiyo maana baadhi ya wanaume hukimbilia kupiga kwa sababu kwa kujibishana kwa maneno siku zote, mwanaume hamuwezi mwanamke! Prove it!
WASIWASI WANGU MKUBWA
Nilijaribu kuchunguza kwa muda mrefu kuhusu wanandoa wanawake ambao walipata mafunzo ya Kitchen Party nikagundua kuwa, wengi wao wanapoingia ukumbini siku ya sherehe mawazo yao ni kutuzwa vyombo tu! Kwamba atatuzwa vyombo vya aina gani?’ Je, vyombo atakavyotuzwa vitavunja rekodi ya alivyotuzwa shoga yake Kidawa wakati anaolewa na Bakari?
Tukutane wiki ijayo kwamuendelezo wa mada hii.
GPL
1 comment:
na wanaume nao pia wafanyiwe kitchen party na send off kwa sababu wako nyumba sana wanategemea mkee apike apakuwe wawe wanalipa bill sawa,awe anamtunza kwa kumbebeleza eti kwa vile yeye ni kichwa cha nyumba mweeeeeeeeeeeeeeeee.mnawazimu.majukumu yote haya ya mwanamke mume kuleta pesa ndani na kila anapotaka kwani mashine hii hachoki.
mfanyiwage na nyinyi kitchen party na send off na mfundwe jinsi yakukaa na mkee.mkee si mtumwa wako ni msaidizi wako tuu na si wakululea wewe kwani kwenu hujalelewa na mama yako.
Post a Comment