Kijana mmoja mkazi wa Kigogo Sukita jijini Dar es Salam ameambulia kipigo kizito kutoka kwa wananchi wenye hasira kali na kufikia hatua ya kutaka kumchoma moto kutokana na kitendo cha kumuibia simu na shilingi elfu therasini mwanadada ambaye naye ni mkazi wa eneo hilo.
Kutokana na kipondo cha aina yake alichokuwa akipewa na wananchi hao wenye hasira kali walionekana kumpania kutokana na vitendo vyake vya wizi wa mara kwa mara na kutokana na kipigi hicho kilichomfanya atapakae damu mwilimzima, mama yake mzazi aliamua kuingilia kati ili kumuokoa mwanaye ambapo naye alionja joto ya jiwe.
Kutokana na timbwili hilo la aina yake, mama huyo aliendelea kumshikilia mwanye huyo kana kwamba aliyekuwa tayari kwa lolote ilimradi amnusuru na kifo.
2 comments:
Very Sad. si vizuri watu kuchukua sheria mikononi mwao, hapo aliyeiba na anayempiga mwizi wote wamekosea. very sad.My heart goes out to his poor mother. As a mom, I can only imagine
JAMBO LA AIBU MTU AMEIBA ALFU THELATHINI TU WAKATI MAWAZIRI WENU MLIOWACHAGUA WANAIBA MABILIONI,WAMAWACJEKA NYIE VIBAKA WANAWAONA WAJINGA
Post a Comment