Maonyesho ya Tanzania Buildex Internatinal Trade Exhibition January 29 -31, yanayoendelea ndani ya ukumbi wa mikutano wa Mlimani City Conference, yanatarajia kufikia tamati jioni ya Jumamosi Januari 31, 2015.
Maonyesho hayo yaliyoandaliwa na kampuni ya kigeni kutoka falme za kiarabu ya S.K.M Air Conditioning LLC na wadau wengine yameshirikisha makampuni zaidi ya 50, ya ndani na nje ya Tanzania ambapo wameonyesha bidhaa zao hizo pamoja na kuuza.
Baadhi ya makampuni yaliyoshiriki kwenye maonesho hayo ni pamoja na kampuni ya huduma za internet ya Simba Net (T) LTD, TRADEX Corporation, Choice International wasambazaji wa bidhaa za Lontor, ISTSL Limited, Rehoboth, Fairy Delights, Afri Vision, Dello Enterprises Ltd wasambazaji wa vifaa vya SKF, SATA Ltd, na mengine mengi.
Makampuni hayo ni yale ya bidhaa za ujenzi, vifaa vya magari, vitu vya ndani, bidhaa za viwandani, maofisini na sehemu mbalimbali pamoja na makampuni ya bidhaa tofautitofauti.
CEO wa TRADEX Corporation, Frank A.P.M Bruurs, akionesha wateja (hawapo pichani) namna ya bidhaa zao zinazopatikana Netherlands na Ujerumani- s-Hertogenbosch. wakati wa maonesho ya Tanzania Buildex Internatinal Trade Exhibition, Mlimani City.
Direct Sales Agent wa SimbaNET, Lilian Godfrey (kushoto) akiwa na Deusdedit Msafiri wa SimbaNET, wakiwa kwenye maonesho ya Tanzania Buildex Internatinal Trade Exhibition, Mlimani City.
Direct Sales Agent wa SimbaNET, Lilian Godfrey akionesha moja ya huduma za SimbaNET FIBER, wanazotoa, wakati wa maonesho ya Tanzania Buildex Internatinal Trade Exhibition, Mlimani City.
Maofisa wa ITS Limited, kutoka India na Tanzania, wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa maonesho ya Tanzania Buildex Internatinal Trade Exhibition, Mlimani City.
Managing Director wa Dello Enterprises Ltd, Daniel Kirahi ambao ni wasambazaji wakuu wa bidhaa za SKF za mitambo ya mashine, magari na vifaa vya viwandani, akionyesha moja ya bidhaa hizo, kwenye maonesho ya Tanzania Buildex Internatinal Trade Exhibition, Mlimani City .
Custormer Support Executive wa kampuni ya SME Ltd wa bidhaa za SATA, Waqas Ahmed akinesha bidhaa za kampuni hiyo kwenye maonesho ya Tanzania Buildex Internatinal Trade Exhibition, Mlimani City.
No comments:
Post a Comment