Hatimaye leo fainali ya Proin Women Taifa Cup itafanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi kwa kuzikutanisha timu za Pwani na Temeke huku Mshindi wa Kwanza katika Michuano hiyo ataondoka na Kitita cha Shilingi za Kitanzania Milioni 3 huku mshindi wa Pili akiondoka na Milioni 1 na Mshindi wa Tatu akiondoka na Kitita cha Milioni 1.
Mashindano ya Women Taifa Cup ni mashindano ya kwanza kufanyika Nchini Tanzania huku yakiwa yamedhaminiwa na Kampuni ya Proin Promotions na Azam.
Katika fainali hiyo mashabiki wataingia Bure huku mechi hiyo ikirushwa live na Azam TV.
Mgeni rasmi katika Fainali hiyo ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mh Dkt Fenella Mukangara ambae atafunga mashindano hayo katika dimba la Azam Complex ambapo mechi hiyo ya fainali itaanza kutimua vumbi saa 10:15 Jioni huku Jonesia Rukyaa refarii mwenye beji ya fifa ndiye atakepuliza kipenga akisaidiwa na Hellen Mduma, Agness Alphonce na Mwanahamisi Matiku huku kamisaa wa fainali hiyo anatarajiwa kuwa Ingridy Kimaro.
Katika Mechi ya Kumtafuta mshindi wa tatu timu ya Ilala itamenyana na Kigoma ambapo mchezo huo utaanza saa 8 Mchana.
No comments:
Post a Comment