Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kilondo Ludewaa.
Mbunge Filikunjombe akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kilondo.
Mwenyekiti wa kata ya Kilondo wa Chadema Bw Edgar Kyula akimpongeza mbunge wa wa Ludewa Deo Filikunjombe kushoto wakati wa mkutano wake kijijini Kilondo
Mbunge Filikunjombe akikabidhi nyavu za kuvulia samaki kwa ajili ya vikundi vya vijana wote Kijiji cha Kilondo na Lusisi Ludewa.
Mbunge Filikunjombe wa tatu kulia akiwa na viongozi wa kijiji cha Kilondo na Lusisi ambao aliwapa nyavu na vifaa vya michezo.
Kikongwe mkazi wa kijiji cha Kilondo akisalimiana na mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe baada ya kumalizika kwa mkutano wake kijijini hapo.
Mtaalam wa umeme akimuelekea mbunge Filikunjombe mambo ya kitaalam baada ya kutembelea maporomoko ya mto Makete ambao utatumika kuzalisha umeme kushoto ni katibu wa mbunge Filikunjombe Bw Stany Gowele.
Mbunge Filikunjombe akitazama mto Makete.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kulia) akiwa katika box huku ameshika tama eneo la kando ya ziwa nyasa juzi alfajiri akisubiri usafiri wa bodi kuelekea Matema wilayani Kyela baada ya kufanya ziara ya siku mloja kijijini Kilondo wengine pichani ni mkurugenzi wa kampuni ya Kilondo Investment Bw Erick Mwambeleko wa pili kushoto ,katibu mwenezi mkoa wa Njombe Honolatus Mgaya na katibu mwenezi wilaya ya Ludewa Bw Felix.
Na matukiodaimaBlog
WANANCHI wa kijiji cha KIlondo kata ya Kilondo wilayani Ludewa mkoani Njombe wamempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa kuwa mbunge pekee katika jimbo hilo kufika kulala chini ardhini kwenye nyumba isiyo na mlango wala dirisha (Pagale) katika kijijini hicho toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961.
Mbunge Filikunjombe na msafara wake wa watu zaidi ya 15 walifika katika kijiji hicho cha Kilondo kilichopo mwambao mwa ziwa nyasa kwa lengo la mbunge huyo kuwaanzishia mchakato wa kupatiwa umeme kupitia shirika lisilo la kiserikali la Kilondo Investment linalofadhiliwa na mradi wa usambazaji vijijini (REA)
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Bw Laurian Kyula alisema kuwa jimbo hilo limepata kuwa na wabunge zaidi ya 5 ila hakuna mbunge ambae alifika na kukubalia kulala katika kijiji hicho kutokana na kuwa na miundo mbinu mibovu na kutokuwa na nyumba ya kisasa ya kulala wageni zaidi ya nyumba za wananchi ambazo nyingi zipo kienyeji zaidi hazina hadhi .
" Kweli tumeshindwa kuamini kuona mbunge anaamua kulala kijiji hapa hata bila kuwepo kwa maandalizi mazuri ya kulala ......tumekuwa na wabunge wengi sana ila wapo baadhi yao hata kukejeli kuwa kijiji hakina hadhi ya kulaza waheshimiwa hadi watakapoboresha mazingira...kati ya viti ambavyo hatukupata kufikiria ni pamoja na kuja kupokea mgeni wa kiwilaya kuja kulala hapa kijijini ila wewe mheshimiwa wetu Filikunjombe umekuwa ni kiongozi wa aina yake" alisema mwenyekiti huyo
Akimpongeza mbunge huyo kwa jitihada zake za kuwasogezea huduma ya umeme kijijini hapo mwenyekiti huyo alisema kijiji hicho ni moja kati vijiji ambavyo vipo mwambao mwa ziwa nyasa na uwezekano wa kuunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa kutoka Ludewa mjini ama Kyela mkoani Mbeya ni vigumu kutokana na kuzungukwa na milima na maji hivyo kwa upande wao waliamini kabisa kamwe hawatakuja fikiwa na huduma za umeme.
" Tunashindwa kujua ni kiasi gani mbunge wetu unavyotuhangaikia kwa mambo ambayo wengine waliotangulia walituhakikishia kuwa ni vigumu kufikiwa na huduma ya umeme kwa kuwa ni porini labda hadi tutakaposogea karibu na vijiji vya nje ya Mwambao kauli ambazo vilitufanya kukata tamaa kabisa kwa umeme kwetu ni huduma isiyo wezekana.....ila tunashangazwa leo kupitia mbunge wetu Jembe Filikunjombe unatuletea wataalam wa kuanza kujenga mradi wa umeme hapa kijijini"
Bw Kyula alisema kati ya mambo ambayo wao hawata kuja kusahau maishani mwao ni utendaji kazi wa mbunge huyo na maendeleo makubwa aliyoyafanya katika jimbo hilo la Ludewa kwa kipindi cha miaka minne ya ubunge wake huku wapo waliokaa miaka mitano bila kufanya jambo linaloonekana kwa wananchi wao.
Hivyo alisema iwapo chama cha mapinduzi (CCM) kitataka kulipoteza jimbo hilo la Ludewa ni pamoja na kujaribu kufanya maamuzi yasiyo hitajika kwa wananchi yakiwemo ya kukata jina la mbunge wao katika mchakato wa kuomba kugombea ubunge jimbo hilo la Ludewa na kumpa nafasi mtu wa kwao watashangazwa na maamuzi magumu ya wananchi kwa kulitoa jimbo hilo upinzani kama fundisho kwa CCM kupenda wanachopenda wao na sio wananchi.
Awali mkurugenzi mtendaji wa mradi wa Kilondo Investment Bw Erick Mwambeleko akielezea mradi huo alisema kuwa mpango wa kuwaunganisha wanakijiji hao na umeme ulikuwepo toka wakati mbunge Profesa Raphael Mwalyosi akiwa madarakani ila cha kushangaza kila alipomfuata kutaka kusaidia kufanikisha kuanzishwa kwa mradi huo aliishia kutoa kauli za kukatisha tamaa kuwa haweza kusaidia kupeleka umeme kijijini hapo kwa kuwa ni gizani sana hakuna faida yoyote .
" Ni kweli kijiji hiki cha Kilondo kipo porini zaidi ila kuna watu wanaishi hata mimi Mwambeleko ni mzaliwa wa hapa hivyo nimesoma sayansi na kutumia elimu yangu nikaona ngoja nishirikiane na mbunge Filikunjombe kuleta ukombozi wa umeme huku kwa kupitia kampuni yangu ya Kilondo Investment kampuni ambayo mchango wa mbunge ni mkubwa zaidi hadi leo tunaanza mchakato wa kuleta umeme hapa....
Alisema kuwa tayari fedha kiasi cha zaidi ya Tsh milioni 300 zimepatikana kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo ambapo fedha hizo kiasi zimetoka REA na nyingine ni fedha ambazo ni mchango wa mbunge Filikunjombe .
Pia alisema umeme huo utazalisha kijijini hapo kupitia maporomoko ya maji ya mto Makete ambayo yanaingia katika ziwa nysa na kuwa maporomoko hayo yana nguvu ya kuzalisha umeme KV 50 na kasi ya maji katika maporomoko hayo ni lita za ujazo 9312 kwa sekunde maji ambayo yanatosha kabisa kwa uzalishaji wa umeme wa kutosha kaya zote kijijini hapo na kijiji cha jirani.
Kwa upande wake mbunge Filikunjombe akielezea sababu ya kulala kijijini hapo alisema kuwa moja kati ya ahadi yake kwa wananchi wa Ludewa ni kufikisha maendeleo kila kona ya jimbo hilo na kuwa akiwa katika ziara pale ambapo jua litazamia ndipo atakapolala bila kujali uwepo wa maandalizi ama lah.
"Wananchi wote wa Ludewa ni wapiga kura wangu hivyo imekuwa ni kawaida yangu kuwa nao wakati wote na kulala popote na kula chochote ambao wao wanakula siku zote .....hivyo jua linapozamia nikiwa ziarani nitalala hapo bila kujali maandalizi lengo kuona nashirikiana na wananchi wangu kwa mazingira yoyote yale......nimefurahi sana leo kulala katika nyumba hii inayojengwa ambayo haina sakavu ,milango wala madirisha (Pagale) mimi ni siufanyi ubunge kama ufalme kuwa nikija mimi ziarani wananchi wangu wasumbuke kufanya maandalizi yasiyo ya kawaida"
Kuhusua mradi huo wa umeme Filikunjombe alisema kuwa lengo lake kuona wananchi hao wanapatiwa umeme mapema zaidi ikiwezekana ndani ya mwaka huu wananchi hao waweze na umeme katika makazi yao hivyo kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa mafundi waliofika kijijini hapo kuanza utekelezaji wa mradi huo pamoja na kuwasaidia kufanya tathimini ya mahitaji ya taa na ufungaji umeme katika nyumba zao.
No comments:
Post a Comment