Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Muwakilishi wa Kudumu wa Jamburi ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi (kushoto) na Naibu Mwakilishi wa Kudumu, Balozi Ramadhan Mwinyi. Mhe Ridhiwani Kikwete ( Mb) alikuwa Jijini New York kwa ziara ya kikazi ambapo pia alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya miaka 38 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinguzi iliyoandaliwa na Tawi la CCM New York na vitongoji vyake.
Mhe. Ridhiwani Kikwete ( Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi na baadhi ya maafisa wa Uwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. Mhe. Ridhiwani Kikwete pamoja na kuhudhuria hafla ya CCM kutimiza miaka 38 pia alipata fursa ya kufika katika Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, fursa aliyoitumia kubadilishana mawazo na Maafisa wa Uwakilishi.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake