ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 24, 2015

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA MHE. JANET MBENE AKUTANA NA WAFANYABIASHARA LONDON

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mama Janeth Mbene (pili kulia), kwenye picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Bwana Msafiri Marwa, msaidizi wa Naibu Waziri Dada Magdalena , pamoja na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London Bwana Yusuf Kashangwa mara baada ya Mhe. Waziri Mbene kuwasilini London, Uingereza kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mama Janeth Mbene, akiongea na Wafanyabiashara na Wawekezaji katika katika Mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya East African Association na Kituo cha Biashara, London. Mkutano huo uliokuwa na lengo la kuwakutanisha Wawekezaji hao wenyenia ya kuwekeza na kufanyabiashara na Tanzania katika sekta mbalimbali kama vile, Kilimo, Umeme, Madini, Elimu na Afya.
Naibu Waziri Janeth Mbene (pili kushoto), Naibu Balozi wa Tanzania, Uingereza, Bwana Msafiri Marwa (wa kwanza kushoto ), Dada Magdalena (Msaidizi wa Naibu Waziri) na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara, London, Bwana Yusuf Kashangwa, wakiwa kwenye Mkutano wao na Wafanyabiashara na Wawekezaji. Mkutano huo uliofanyika jana jumatatu, tarehe 23 Februari 2015. Picha na Ally Dilunga

Naibu waziri wa viwanda na biashara Mheshimiwa Janet mbene katika siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi nchini Uingereza, amekutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara na wawekezaji kupitia Chama chao cha East African Association, yenye lengo la kuvutia uwekezaji katika viwanda na kuongeza thamani bidhaa zinazozalishwa Tanzania.

Mheshimiwa Mbene amewaeleza wafanyabiashara hao hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara, hasa kwa kufanya marekebisho ya mifumo ya utoaji huduma za kiserikali kwa wafanyabiashara na wawekezaji nchini kupitia kitengo kilichoko katika Ofisi ya Rais kijulikanacho kama “Presidential Delivery Bureau” kinachoongozwa na Mtendaji wake Omari Issa.

Aliwaambia wafanyabiashara hao kuwa licha ya kurekebisha mifumo hiyo pia kinalenga kuondoa migongano ya kisheria na ya kiutendaji iliopo miongoni mwa Taasisi za Serikali kama za Mamlaka mbalimbali kama ya Mapato (TRA) na zinginginezo kama BRELA, na TIC, na zingine zinazohusika na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wafanyabiashara.

Aliwaambia kuwa kupitia PBD, kulipendekezwa sekta kipaumbele ambazo zimewekwa katika Mpango wa utekelezaji wake wa Matokeo Makubwa Sasa au “BIG Result Now”. Alizitaja Sekta hizo kuwa ni za Nishati, Kilimo, Maji, Miundombinu, Elimu na utaratibu wa upatikanaji wa Rasilimali.

Alisema kuwa watendaji katika sekta hizo walipewa malengo ya utekelezaji na kwamba baada ya tathmini ya mwaka mmoja sasa, hali inaonyesha kuwa utekelezaji wa programu hiyo unaenda vizuri na umeonyesha pia kwamba kumbe hatua za kurekebisha mifumo ya utendaji kazi wa serikali zinawezekana.

Aliongeza kusema kuwa kutokana na mafanikio hayo ya muda mfupi, Wizara yake ya Viwanda na Biashara nayo pia imeingizwa katika Mpango huo ili kuharakisha urekebishaji wa mifumo ya utoaji Leseni, Vibali na huduma nyingine za biashara. Lengo likiwa ni kuwezesha utoaji huduma hizo katika mifumo ya kigitali kupitia Mtandao ili kuondoa tuhuma za rushwa na kuharakisha utoaji wa maamuzi.

Mheshimiwa Mbene ametumia pia fursa hiyo kuwahamasisha wawekezaji kuwa wakati Serikali inaendelea kurekebisha mifumo yake ya utoaji huduma, waje kuwekeza nchini hasa katika viwanda vya kusindika mazao ya kilimo na bidhaa nyingne kama madini kupitia Maeneo maalum ya uzalishaji (yaani EPZs na EFTAs), ambayo yametengwa tayari katika mikoa kadhaa ambayo ni muhimu katika kufanikisha malengo ya kiuchumi.

Ameyataja maeneo hayo kuwa yapo katika mikoa ya Mtwara, Dar es Salaam, Bagamoyo, Tanga, Ruvuma, Kigoma, Arusha na Kagera.Licha ya kuyataja maeneo hayo, Mheshimiwa Naibu Waziri aliwaeleza wafanyabiashara hao kuwa pia zipo fursa za kutosha za uwekezaji nchini Tanzania katika sekta mbalimbali kama miundombinu, nishati (hasa nishati mbadala za jua na upepo), kilimo hasa cha mazao ya nafaka kama mchele, mahindi, miwa, n.k.

Alizitaja sekta zingine kuwa ni za utaoaji huduma kama za Utalii (katika ujenzi wa Mahoteli), Hospitali na Shule (katika kuboresha elimu).Kesho Mheshimiwa Naibu Waziri anatarajia kukutana na watendaji wa Kampuni ya SACOMA inayoagiza bidhaa za mbogamboga, matunda na Maua kutoka Afrika

No comments: