ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 24, 2015

NGUMI KUPIGWA FEB 28 UWANJA WA NDANI WA TAIFA


'

BONDIA Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe'  ametamba kumsambalatisha Fadhili Majiha
Stoper' katika raundi za awali za mpambano wao utakaofanyika siku ya jumamosi ya feb 28 katika uwanja wa ndani wa taifa mpambano huo wa raundi nane unasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki mbalimbali wa mchezo wa masumbwi nchini ususani vitongoji vya Kinondoni, Manzese, mabibo na Mwananyamala ambapo ndio maeneo yao yenye wapenzi wao wa ngumi na sehermu mbalimbali

akizungumza na mwandishi wa habari hizi Miyeyusho ametamba kuwa atokuwa na mzaha siku hiyo itakuwa kazikazi mana yeye ni bondia mkubwa sana hapa nchini na akuna mtu wa kumbabaisha kwa sasa katika uzito wake

mbali na mpambono huo wa utangulizi kutakuwa na mpambano wa ubingwa wa U.B.O Africa utakaowakutaniosha mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Cosmas Cheka kutoka Morogoro ambao watatanguliwa na mapambano mengine yatakayowakutanisha Shomari Mirundi zidi ya Mwinyi Mzengela wakati Shedrack Ignas atapambana na Husein Mbonde, na Godfrey Slive atamenyana na Sadick Abdulazizi
siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali

na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

No comments: