Saturday, February 21, 2015

Naungana na Wewe Kupinga Vitendo vya kikatili juu ya Albino

"Ni kweli mimi ni Albino, nimejikubali na nimeishi maisha yangu yote bila kujali nilivyo. Sijawahi kutumia hali yangu kupata kitu kwa huruma, nimeyapigania maisha yangu na nimepiga hatua.

Leo hii naongea nanyi nikiwa Baba, Mume, Mwandishi Mwandamizi, Blogger, na mengine mengi, lakini hali yangu sasa inaanza kunikwaza.

Haya mauaji jamani, nimejiteua kuwa Balozi, nitatetea, na kusimama mbele ya wenzangu wote wenye hali kama hii, kama ni wanasiasa ama wafanyabiashara, wanataka kutuua kwa maslahi binafsi, mwaka huu HAPANA.

Wanaoniunga mkono mikono juu" Mwisho wa kunukuu.

Nikiwa kama Blogger na Mwanahabari Mwenza wa rafiki yangu na Kaka yangu Kipenzi,Henry Mdimu aliejitolea kuwa Balozi,nanyoosha mkono juu kwa kuunga mkono kupiga vita vikali mauaji ya ndugu zetu wenye Albinism.kwani wao pia ni Binadamu kama tulivyo mimi na wewe.
SISI KWA PAMOJA TWAWEZA

1 comment:

  1. God bless you, tunakuunga mkono nakukusupport.unyama mkubwa sana, bongo uchawi mwingi sana.baada ya kufanya kazi kwa bidii uchawi tu.hadi hapa USA wabongo bado wanaamini uchawi wanatuma hela kwa waganga Sao. Stop it isn't working.work hard, believe God

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake