Sunday, February 22, 2015

SHEREHE ZA MIAKA 38 YA KUSHEREHEKEA KUZALIWA KWA CCM ZA NOGA KAMA MCHARO NEW YORK LICHA YA THELUJI KUNYESHA SIKU MZIMA

 MH. Ridhiwani Kikwete akiongea kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi CCM sherehe zilizofanyika New York na kudhuliwa na wageni mbalimbali kutoka kila sehemu yenye tawi la CCM hapa Marekani.
 MH. Ridhiwani kikwete akiongea mbele ya wa Tanzania waliojitokeza kwenye sherehe hizo za kusherehekea miaka 38 ya kuzaliwa CCM na kuwapongeza kwa kujitokeza ingawa kulikuwa na theluji siku mzima.
 Mwenyekiti wa tawi la CCM New York akiongea kwenye sherehe hizo
 Bwana Isaac Kibodya akiongea kwa niaba ya katibu mwenezi wa tawi la CCM New York

Hapa ni Joyce akiongea wasifu wa Mh.Ridhiwani Kikwete historia yake kwa ufupi
Mh.Ridhiwani akiwa kwenye meza pamoja  na mabalozi wa umoja wamataifa, viongiozi wa tawi na Jumuhia ya Watanzania New York.
Kwa picha zaidi kujionea mambo yalivyo kuwa yamenogo nenda soma zaidi.

Pia waweza kuziona picha za kutoka kwenye sherehe hii kwa kutembelea

8 comments:

  1. Jamani mbona hatujawaona wakali wa DMV,ingekuwa Dmv hapo wote wangevaa kijani ,achana na DMV .DMV ni mwisho.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hamna lolote mmezoea kusikika nyie tu DMV sasa ni zamu ya wana CCM New York. Nyie mnadhani kwamba hakuna tawi lolote la CCM Marekani wanaoweza kufanya shughuli za kichama zaidi ya DMV, sasa wana CCM New York wamethubutu na wameweza, wameshikamana na kufanikisha hii shughuli na kwa style yao, nyie vaeni kijani na njano na wenzenu watavaa chochote ilimradi tuu shughuli husika imefanyika na kufanikiwa. CCM OYEEEEEEEE! !

      Delete
  2. DMV hatupati kigugumizi kurusha kijani na njano. Hawa wezetu vipi? Ama machadema yaliyojificha?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aliyekudanganya kuwa ukivaa kijani na njano ndio CCM nani? Unaweza kuvaa hiyo kijani na njano na bado ukawa mpinzani wamethubutu na wameweza acheni unafiki.CCM New York mmejitahidi sana kazi nzuri ukizingatia ni tawi changa na mara yenu ya kwanza kufanya shughuli rasmi za kichama.Big up wanaccm New York City

      Delete
  3. DMV Kila siku wao wanawapata wageni hawa so this time ni zamu ya watu wa New York waacheni nao wastarehe.sio kila kitu Dmv si wanaye mheshimiwa wao na wajichanganya naye tu.vibahasha vinaishia New York this time.Bora hawajakuja hao DMV.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Well said,CCM New York Ni Tawi changa, wamethubutu na wameweza. Hao wanaojiona kama wao ndio CCM damu na wao walianzia huku huku sasa hivi wanajidai kupiga kelele. CCM bila DMV inawezekana!!!

      Delete
  4. nyie watu wa DMV your negativity won't get you no where.sio kila jambo kuongea trash..wote sisi ni wamoja!ila poleni sana maana maradhi mabaya sana hayo na naamini si wote ila baadhi yenu..!kuweni matured!ujinga ujinga hauna maana!

    ReplyDelete
  5. Comments zote hapo juu ni beneath dignity ya CCM. Mbona u are falling in the trap ya wale ambao wangependa kuona mmegawanyika. Sasa hoja zote ni kwenye mavazi na kusahau mafanikio na ujumbe wa sherehe yenyewe kwamba ilikuwa about Tanzania na Umoja wetu kama Watanzania! NY Oyee, CCM Oyee na Tanzania Oyee!

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake