Friday, February 20, 2015

TANZANIA YAJITAYARISHA KUINGIA KWENYE UCHUMI WA GESI ASILIA

 Siku ya kwanza Prof Muhongo alipoanza kazi akiwa Waziri wa Nishati na Madini alisema (APRIL 2012): “

RASLIMALI ZETU ZITAKUWA SALAMA KWA MANUFAA YA WATANZANIA WOTE IWAPO NCHI YETU ITAPATA WATAALAMU MAHIRI NA WENYE UELEWA MKUBWA KWENYE SEKTA ZA MADINI, GESI ASILIA NA MAFUTA.” 

Prof Muhongo ameendelea kusisitiza kwamba ili tuingie (Tanzania) kwenye Uchumi wa Gesi kwa uhakika na umakini mkubwa lazima tupate Wataalamu mahiri wa Ki-Tanzania kwenye maeneo yafuatayo ya gesi asilia na mafuta: (1) Earth Sciences – geology, geophysics, etc (2) Engineering – all disciplines (3) Law, (4) Finance - Accountancy & Auditing, (6) Environment and (7) Communication experts.

Kwa muda mfupi sana wa miaka miwili na nusu, Prof Muhongo amefanya makubwa sana kuhusu upatikanaji wa Watanzania wenye elimu nzuri, utaalamu, weledi na uzoefu kwenye Sekta nyeti ya gesi asilia na mafuta
.

Kwenye Bajeti za Mwaka 2013/14 na 2014/15, Prof Muhongo aliwatangazia Watanzania, “Marshall Plan” yaani Mradi Mkubwa wa kusomesha vijana wa Watanzania kwa kasi na umakini mkubwa ili baada ya miaka 5 (2012-2017) Tanzania ipate wataalamu wake wenyewe wasiopungua 500. Prof Muhongo aliamua kushirikiana na Vyuo Vikuu vya Dar Es Salaam (UDSM), Dodoma (UDOM), na Arusha (Nelson Mandela) kuanzisha mafunzo kwa ngazi ya shahada (BSc & MSc) hapa nchini. Vilevile aliagiza Chuo cha Madini Dodoma kianze mafunzo ya Diploma (Technicians) ya Mafuta na Gesi Asilia. Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ikitoa “scholarships” au kusaidia kupatikana kwa “scholarships” kuwezesha baadhi ya vijana wetu kupata mafunzo haya. Takwimu ni hizi hapa:

UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM (JUMLA 115

BSc & 13 MSc) BSc Petroleum Chemistry: Year II (24), Year I (20)

BSc Petroleum Geology: Year II (15) Year I (15), MSc Petroleum Geology (13)

BSc Petroleum Engineering: Year II (23), Year I (18)

UNIVERSITY OF DODOMA (JUMLA 134 BSc) BSc Petroleum Engineering: Year IV (4), Year III (52), Year II (36), Year I (42)

MINERAL RESOURCES INSTITUTE- MADINI DODOMA (JUMLA: 357 Diploma in Petroleum Geosciences)

Year III (63), Year II (112), Year I (182)

Wizara ya Nishati na Madini ilihakikisha kwamba eneo la mgodi wa Nzega uliofungwa linapewa Chuo hiki ili kiweze kutoa mafunzo kwa vitendo zaidi na kupanuka. Prof Muhongo amekiunganisha Chuo hiki na Vyuo vya Alberta na Calgary, Canada ili kiweze kutoa mafunzo yanayotambulika ulimwenguni baada ya kuwa POLYTECHNIC kama zile za Canada na kwingineko.

NELSON MANDELA UNIVERSITY, ARUSHA: MSc (Oil & Gas) Matayarisho yamekamilika na huenda wanafunzi wataanza masomo mwaka huu (2015). DIT nao wanajitayarisha kutoa mafunzo ya Diploma kwa Technicians wa mafuta na gesi asilia.

VYUO VYA NJE (BSc): VIJANA WA TANZANIA WANAOSOMESHWA NA WAZAZI WAO NCHI ZA NJE (JUMLA 70 BSc, January 2015)

Kwa kugundua umuhimu wa kupata wataalamu Watanzania kwenye maeneo ya mafuta na gesi asilia, Prof Muhongo alijitahidi kupata takwimu za vijana wetu wanaosomeshwa na wazazi wao nje ya nchi. Hadi kufikia JANUARY 2015, VIJANA 70 wako masomoni China, India, Russia, Malaysia, UK na USA.

WATANZANIA WENYE SHAHADA ZA JUU (MSc & PhD – Oil/Gas)

Kwa kutumia taaluma, uzoefu na uhusiano wake mzuri wa kimataifa, Prof Muhongo alitafuta nafasi za masomo ya ngazi za juu (post-graduate) kwa ajili ya vijana wetu. Vilevile Wizara ya Nishati na Madini ilitoa “scholarships” kwa wafanyakazi wake na kutoka Wizara nyingine kwenda nje ya nchi kusoma Masters za Oil/Gas (km oil/gas masters kwa wanasheria wa AG 4, VP 1). World Bank imetoa fedha nyingi kuunga mkono jitihada za Wizara za kusomesha wataalamu wa mafuta na gesi asilia nje ya nchi. Hadi January 2015, idadi ya vijana wetu wanaosoma vyuo vya nje ni hii hapa

: (1) Norway: Masters 40, ifikapo 2016
(2) China: Masters 18, PhD 2
(3) Uingereza: Masters 20, kwa nyakati tofauti
 (4) Brazil: Masters 5-15
(5) Canada: Makubaliano yatatekelezwa kuanzia mwaka huu (2015)

SERIKALI YA CHINA: Prof Muhongo aliomba scholarships 20 kila mwaka kwa miaka 5 (Jumla: 100) na amekubaliwa. Kati ya February na April 2015, vijana wa Tanzania watakaribishwa kutuma maombi ya kwenda kusoma China ifikapo Septemba 2015. Kwa hiyo wanafunzi 20 wataenda China ifikapo Septemba 2015.

SIR WINSTON CHURCHILL (1874-1965) AKITOA HOTUBA YAKE HARVARD, USA TAREHE 6 SEPTEMBA 1943 ALISEMA, 

“THE EMPIRES OF THE FUTURE ARE THE EMPIRES OF THE MIND.” 

TUJIFUNZE KUTOKA MATAIFA MENGINE: 

Takwimu zinaonyesha kwamba wanafunzi wanaofuzu masomo ya ENGINEERING ya shahada ya kwanza (BSc Engineering) kila mwaka nchini USA ni takribani 70,000, India ni 350,000 na China ni 600,000.

Wawekezaji wakubwa kwenye utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asilia nchini mwetu ni kutoka Norway, UK na USA. Takwimu zinaonyesha kwamba watafiti nchini mwao ni wengi sana: Number of Researchers in R&D per million people (namba ya watafiti kwa kila watu milioni moja nchini mwao) in 2010 in Norway was 5,408. UK 4,134 and USA 3,838. Tanzania was 36. Tukijilinganisha na majirani zetu kwa mwaka 2010: Uganda was 37 and Kenya 227. South Africa ilikuwa na 364, LAZIMA TANZANIA ISHINDANE, ISIACHWE NYUMA!

Prof Muhongo ameendelea kusisitiza umuhimu wa SCIENCE, MATHEMATICS, ENGINEERING kama msingi wa kupata Watanzania mahiri kwenye mambo ya TEKNOLOJIA na UBUNIFU (INNOVATION) kwa manufaa ya ustawi wa Taifa letu KIUCHUMI NA KIJAMII. Takwimu za wataalamu Watanzania kwenye Sekta ya Gesi Asilia na Mafuta inatia matumaini makubwa. Hadi January 2015, takwimu zinaonyesha:

(1) UDSM: 115 BSc & 13 MSc students
2) UDOM: 134 BSc students
(3) OVERSEAS UNDERGRAGUATE(70+20 China/2015) POSTGRAUATE (85) students
(4) MADINI INSTITUTE: 357 Diploma students

Idadi ya wafanyakazi wataalamu (Watanzania) wa TPDC ni kama ifuatavyo:

(1) PhD = 7, (2) MSc/MA =65, (3) BSc =205 (4) Technicians =75

Tanzania kuwa na jumla ya wataalamu wa gesi asilia na mafuta wasiopungua 500 ifikapo 2017 kama ilivyopendekezwa na Prof Muhongo INAWEZEKANA.

 “THE EMPIRES OF THE FUTURE ARE THE EMPIRES OF THE MIND.” 

1 comment:

  1. On paper it sounds good but kwenye profit only a few benefit......

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake