Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Maendleo ya Jamii Bw. Xavier Keebwe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa vijana kuhusu Sera ya maendeleo ya Vijana, Stadi za Maisha,Ujuzi, Mwongozo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana yaliyotolewa na wawezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambapo jumla ya zaidi ya Vijana 60 kutoka katika halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijini mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbvi wa manispaa hiyo.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akitoa mada mbele ya Vijana kutoka Halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijijini katika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada mbele ya Vijana kutoka Halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijijini katika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Baadhi ya Vijana wakifuatilia mada wakati wa warsha iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kuhamasisha vijana kuhusu Mfuko wa maendeleo y Vijana nchini. Warsha hiyo imefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo jumla ya zaidi ya vijana 60 kutoka katika halmashauri za Manispaa hiyo, Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijijini.
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Peace Group kilichopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Bibi. Cecilia Alphonce walipotembelea kikundi hicho kwa ajili ya kukagua shughuli zao mkoani Kigoma.Kikundi hicho kinajishughulisha na uzalishaji wa miche ya miti na maua na kinaundwa na wanachama watano.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akisikiliza maelezo kuhusu uzalishaji wa miche ya maua kutoka kwa mmoja wa wanakikundi cha Peace Group kutoka Manispaa ya Kigoma Ujiji Bibi. Angelina G. Masunzu leo wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya Vijana mkoani Kigoma.
1 comment:
Poa Sana
Post a Comment