Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akimpokea Mwanzilishi wa Taasisi ya Maendeleo ya Aga khan Duniani, Mtukufu Karim Aga Khan mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mtukufu Aga Khan yupo nchini kwa ziara binafsi ya siku nne, ambapo pia atatumia fursa hiyo kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya taasisi hiyo hapa nchini.
Mtukufu Aga Khan akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Nchini Dkt. Shukuru Kawambwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Mtukufu Aga Khan akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Mindi Kasiga mara baada ya kupokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Ijumaa tarehe 20.02.2015
Mtukufu Aga Khan akisalimiana na Afisa Mambo ya Nje Hassan Mwamweta baada ya kuwasili jijini Dar es salaam kwa ziara ya siku nne nchini Tanzania.
Waziri Membe akizungumza jambo na Mtukufu Aga Khan mara baada ya sherehe fupi ya mapokezi baada ya kuwasili nchini.
Picha na Reginald Philip
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake