ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 3, 2015

WIZARA YAWATAKA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI KUWAKATIA BIMA WAFANYAKAZI WAO

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia akijibu swali Bungeni mjini Dodoma.
Na Lorietha Laurence-Maelezo Dodoma.


Naibu Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia amewataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwakatia wafanyakazi wao bima ili ziweze kuwasaidia wakati wanapopatwa na madhara wakiza kazini.


Akijibu swali la mbunge wa viti maalum Anna Mallac, kuhusu mpango wa Serikali kuwapatia ulinzi waandishi pale wanapokuwa wakifanya kazi katika matukio hatari, Naibu Waziri Nkamia alisema kuwa serikali inafahamu mazingira ya kazi ya wanahabari na inawajibika kikatiba katika kutoa ulinzi kwa raia wake wote wakiwemo wanahabari.


“Uandishi wa habari ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine muhimu katika jamii kama ilivyo taaluma ya sheria ualimu na udakatari na ni muhimu kufahamu na kuzingatia miiko ya taaluma pale wanapokuwa katika eneo la kazi”alisema Nkamia.


Aidha alibainisha kuwa jukumu la kwanza kwa waandishi wa habari ni kujilinda na kujihami wao wenyewe kwa kuwa wanayafahamu mazingira yao ya kazi na pia kuzingatia miiko ya taaluma yao kwa kuangalia wanayotakiwa kufanya na kutofanya katika eneo husika. Aliongeza kuwa wanahabari wanatakiwa wazingatie sheria bila shuruti kwa kuwa nao ni wananchi kama walivyo wananchi wengine na hakuna aliye juu ya sheria .


Hata hivyo Serikali imekuwa ikiwapatia waandishi wa habari vifaa maalum katika matukio mbalimbali ya kitaifa ikiwemo vitambulisho na mavazi maaalum ya kuwatambulisha wakiwa katika eneo la kazi ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuwalinda na madhara yeyote.


Naibu Waziri Nkamia alieleza kuwa kwa sasa wizara yake imekuwa ikiandaa muswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao utawasilishwa mbugeni wakati wowote kuanza sasa. 
SOURCE:JIACHIE

No comments: