Imeandaliwa na John Haule wa Rumours Africa
Mstari wa rizki katika Wiki jana tuliuzungumzia mstari wa maisha au Life Line. Tuliona faida za kuutumia mstari huo kujijua ulivyo na kujua unatakiwa ufanyaje ili kufanikisha mambo yako maishani, na pia tuliona hasara za kutojua kuusoma mstari huo pia.
Wapo walionipigia kutaka kujua kuwa niliwezaje kujua rais wa zamani wa Libya Kanali Muhammar Gadaffi, na rais wa zamani wa Uganda Idd Amin Dada wana alama nilizowatajia ilihali si rahisi kuwasogelea marais na kuwasoma viganja vyao? Swali hili nilijua lingewasumbua wengi japo hamkunipigia kuniuliza. Ni kwamba kwa kawaida mikono na viganja vya watu maarufu wakiwemo maraisi vipo kwa ajili ya kupungia watu zaidi ya kufanya kazi nyingine! Viganja vyao vinasomwa kwa urahisi mno kila wanapohutubia popote waendako.
Wakati fulani niliwahi kuandika mstari huu wa riziki au Head Line huku nikimhusisha Mheshimiwa rais Dr. Kikwete, na mmiliki wa timu ya mpira barani Ulaya Chelsea FC. Bw. Abromovich ambapo niliwaasa watanzania watulie kwa kuwa tupo katika viganja salama vya rais wetu huku nikiwaasa wapenzi wa Chelsea FC. Kuwa mmiliki wa timu hiyo ni mtu mwenye taswira tofauti na rais wetu kwa kuwa yeye ni mtu anayetumia nguvu kutoa maamuzi kwa hiyo ipo siku atajichanganya na timu itamshinda, maana tayari tunasikia “special one” anarudi England…
Lakini Dr. Kikwete ni tofauti, mstari wake wa riziki ni ule ambao kwanza haufanani na umbo la kiganja chake. Yeye mstari wake umejichimba kiasi cha kutosha kuusoma wazi ili kuthibitisha kuwa yeye ni mtu mkweli, sahihi na anayeona mbali sana na ndio maana siku zote huthibitisha kuwa yupo WAZI kwa kutabasamu akiongea ilihali ni machungu na hata matamu popote bila wasiwasi.
Nakumbuka aliwahi kukaririwa akisema sura yake “isitudanganye” tukafikiri ndivyo alivyo. Mstari wake wa riziki unafanana sana na ule wa rais wa Marekani Barack Obama hata ukiwaangalia tu viganja kwa macho na ndio maana wengi hawaamini imekuwaje “Jaluo” awatawale watu jeuri kama Wamarekani. Lakini wajanja siku zote hunasa katika tundu bovu maana Wamarekani hao hao siku moja walijishangaa pale Abraham Lincon walipoiweka sura yake katika noti yao US Dollar, huku akiwa ni mtu pekee ambaye hajawahi kuwa rais kama wengi tulivyozoea…
Lakini msisahau kuwa nilianza habari hii kwa kuuelezea mstari wa majanga. Hata rais naye anao mstari huu ili mjue kuwa hata Mungu hakupi kitu usichoweza kukibeba! Yeye mstari wake umenyooka na unaonekana wazi kabisa kuthibitisha kuwa ni mmoja kati ya wachache duniani ambao wana uwezo wa kuyabeba majanga makubwa ya dunia hii mabegani mwake huku akitabasamu daima.
Lakini, hebu tujiulize mstari wa riziki au wengi huuita wa busara ni upi? Huu ni msatri unaoanzia kati ya kidole cha shahada na kidole gumba. Inawezekana kabisa mistari ya maisha na riziki ikakutana lakini haigandani pamoja bali huachana palepale inapokutana na wengine hugandana kwa sentimita kadhaa.
Kama mstari wako wa riziki ni mfupi basi ujijue kuwa huna uwezo mkubwa wa kufikiri na kazi za akili zitakushinda. Lakini kama mstari wako wa riziki ni mrefu sana basi ujijue kuwa kugombana na watu kwa kuwaona ni wajinga hukutokea sana na ni bora ukajifunza kukaa kimya unapoona jamii inakubaliana na jambo ambalo wewe unaona wanakosea. Kama ni la hatari basi kaa mbali nao maana watakuponza! Lakini ukiona mstari huo kwako ni mwembamba umezama sana kiganjani na unaonekana kwa uwazi sana basi uwezo wako wa kuona na kujua mambo ni mkubwa kuliko yeyote pale ulipozungukwa na jamii.
Kama mstari huo una viduara-duara, basi ujue kuwa wewe si mtu makini, hukumbuki mambo yako na inawezekana kabisa ukawa na hitilafu za wazi katika ubongo ikiwemo wehu, utaahira, ajali ya ubongo nk. Lakini pia kama unaona viduara vimeungana kama mnyororo pale unapoanzia mstari huo basi ujue kuwa uwezo wako wa kujua na kupambanua mambo katika maisha yako ikiwemo elimu vitavurugwa au vimevurugwa na mazingira magumu unayokabiliana nayo.
Mstari huo wa busara au riziki unaweza gusana na ule wa maisha inapokutana mistari hii kama nilivyosema hapo juu. Ukiona mstari wa riziki unaugusa wa maisha halafu mistari inaachana mara tu inapogusana basi ujue umejipanga kimaisha, mwangalifu sana, mtu wa vitendo sio maneno, lakini kama mistari hiyo imegusana kwa sentimita kadhaa basi wewe ni mwoga na mwenye wasiwasi mara zote na sio wa kuwaongoza wenzio hasa katika mambo yanayotaka kiongozi jasiri.
Kama mistari hiyo imeanza sehemu moja ikakutana na ikaendelea bila kukutana hadi mwisho basi wewe ni mtatuzi mzuri wa matatizo na suluhu za waliyoshindwa wenzako na hata muonekano wako ni wenye heshima kwa jamii kwa kuwa unaweza kuikumbatia hatari kubwa na kujua namna ya kupanga na kuimaliza hatari yoyote huku watu wakibaki na mshangao mara zote bila kujua umefanyaje.
Kama mistari hiyo haijakutana toka mwanzo hadi mwisho basi ujijue kuwa wewe si mwoga! Una akili za ziada katika jamii inayokuzunguka na una uwezo wa kuelezea jambo mbele ya kundi la watu bila woga na ukaeleweka zaidi ya yeyote
Wiki ijayo tutazungumzia aina za viganja na namna unavyoweza kumsoma mtu bila kukufunulia kiganja chake. Lakini pia tutakapo pata tena nafasi katika siku zijazo basi tutazungumzia pia namna ya kujua mtu mwenye mistari ya aina Fulani kwa kauli zake na vitendo vyake tu. Kwa leo naishia hapa na wote wenye shauku ya kujua kitu au kutoa maoni wasisite kuwasiliana nami kwa simu au email na wenye shauku ya kusomwa viganja nawakaribisha ofisini wasisite kuja.
Mwandishi wa Makala hii anapatikana kupitia Email ya: rumoursafrica@gmail.com au Simu Namba +255 768 215 956
No comments:
Post a Comment