ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 17, 2015

Kakobe :Rose Muhando Sio Mlokole Hata Kidogo Anawakatisha Wanaume Viuno Stejini

Kiongozi wa Kanisa la Full Bible Gospel Fellowship, Askofu Zakaria Kakobe Amewalipua baadhi ya Wanasiasa na waimbaji wa Injili wanaotumia neno uokovu katika maisha yao wakati haipo hivyo...
Askofu Kakobe aliyasema hayo alipokuwa akihubiri kanisani kwake na kumtolea mfano Mwimbaji Rose Mhando na kusema hana sifa za ulokole kwa kuwa anawachezesha wanaume kwa kukata mauno kwenye nyimbo zake , Amesema "Hivi kweli mtu kama Rose Muhando unaweza sema ameokoka ..embu tuache utani na kumrudia Mungu Jamani"


8 comments:

Anonymous said...

mbona anachoyo cha roho huyu kakobe ndo hilo ameliona kubwa mbona hasemi wanaowatafuta wake za watu wakienda kuombewa maombi ya private na kuzaa nao,mbona hawasemi wanaowabaka watoto,mbona hayo ni maofu kupita yote yeye anasema wanaume kukatika ndo anaona ya muhimu.mwaafyuuuuu

mbona hasemai mtu akija amenona akitoa sadaka kubwa ndo anaheshimiwa kuliko anayetoa sadaka ndogo.mbona hasemi usanii wanaofanya wakuwatoa watu mapepo wakati wao ndo wamewatia hao mapepo.mwaaafyuu.

UTAWAJUA KWA MATENDO YAO.

tumuogope mungu kwa mengi tu na si haya ya kukatika viuno japo si mema.

Anonymous said...

huyu naye kakobe anahitaji arudi msalabani akaokoke tena mara ya pili nimesikiliza kwenye audio clip yake nikaona kawakweza wenzake anatakiwa awaite awaonye na kuwakataza si eti leo kuwatusi mbele ya kondoo.

Ni Nani aliye na hakika kuwa kweli ameokoka hapa duniani?Dunia ina Siri nyingi mno.Tukifika hapo tumwachie Mungu.Aliyeokoka anasema uongo?

kwenye audio clip hiyo kamtaja mpaka kikwete kwamba hajaokoka cha kushangaza kwani kikwete kasema kaokoka yeye na yeye si muislamu si anaruhusiwa kuwa na wake zaidi ya mmoja au hilo halijui.

luke na vijimambo team wawekeeni hiyo clip wadao wengine waisikilize au wambiiye waje bongo.

Anonymous said...

utawajua kwa matunda yao walio okoka kweli.

kakobe awachana ma agent wa albino.hamjali mwana siasa yeyote yule kwa sababu hapokei msaada wa pesa kutoka kwao yeye anamtegema mungu na kumtegemea yeye ndo mpago wake mzima.

ma agent wa albino watafura na kupasuku shauri yao kakobe ndo kishawachana live.

Anonymous said...

ni kweli kabisa hana maadili mema wala heshima

Anonymous said...

Haaa ati arudi msalabani akaokoke mara YA pili....!!!
Dashes tu wanamadongo sana!!

Anonymous said...

Mungu mwenyewe ndiye ajuaye mtu anayemtegemea. Hakuna mwenye haki hapa duniani ha huwezi kumsema mtu hayuko kamili maana wewe sio muumba. Inaelekea huyu mchungaji hajaelewa neno.

Anonymous said...

Kakobe naye mkristo au business man. Jamaa hata dini hana

Anonymous said...

Hakuna mchungaji hata mmoja alieokoka bongo wote zuga tu so wee kakobe wacha kumnyooshea kidole mwenzio hata wewe ni mchafu tu,kwenda zako huko