Mhe. Waziri Sophia Simba akiwa na Mhe. Halima Mdee, Katibu Mkuu Anna Maembe, na Balozi Tuvako Manongi katika moja wa mikutano ya pembezoni iliyokuwa inakwenda sambamba na majadiliano ya jumla ya Kamisheni ya 59. Mkutano huu uliandaliwa na Mke wa Rais wa Kenya Mama, Margaret Kenyata, ambapo alitumia fursa hiyo kuelezea shughuli anazozifanya za kuwasaidia wanawake na watoto wa nchi mwake hasa wale walio katika mazingira magumu. Kampeni yake inayoitwa Beyond Zero inalenga katika kufikisha huduma za afya
Mhe. Waziri Simba akisalimiana na First Lady wa Kenya Mama Margaret Kenyata, First Lady huyu hukimbia mbio za marathon kama njia moja wapo ya kufatua raslimali za kuwasaidi akina mama wenzie na watoto walio katika mazingira magumu.
Mhe. Waziri Simba na Balozi Tuvako Manongi wakibalishana mawazo
Pamoja na kuhudhuria mbalimbali inayohusianana Kimesheni Kuhusu Hadhi ya Wanawake, Mwakilishi wa Kudumu wa wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, alipata fursa ya kuwapokea na kuzungumza na wageni mbalimbali waliofika katika Uwakilishi wa Kudumu. katika picha zifuatazo Balozi Manongi akiwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walikuwa Jijini New York kwa shughuli za Kikazi.
Utanzania na uzalendo kwanza" ndivyo anavyoelekea kusema Mhe. Susan Lymo wakati yeye na wabunge wenzie walipofika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu Hadhi ya Wanawake, kwa wiki kuanzia jumatano hadi Ijumaa wameendelea na jukumu kubwa la kujadiliana, kuhabaridha,a kubadilishana uzoefu, kuelimisha na hata kujifunza namna ya kuzikabilia changamato mbalimbali ambazo mwanamke na mtoto wea kike wanaendelea kukabiliana nazo. Mkutano huu wa mbao ni wa waki mbili unafanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 20 tangu kufanyika kwa mkutano wa kihistoria wa wanawake uliofanyika mwaka 1995 huko Beijing, China.
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar unaongozwa na Mhe. Sophia Simba ( Mb) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na umekuwa ukishiriki majadiliano ya jumla na mikutano ya pembezo iliyobena maudhui mbalimbali lakini yote yakilenda katika usawa wa jinsia na uwezeshwaji wa mwanamke.
No comments:
Post a Comment