NI ARUSHA
Tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Triple A, jijini Arusha ambapo mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006 alienda kwenye sherehe ya mmoja wa rafiki zake huku yeye akipewa ‘taito’ ya mgeni rasmi.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kilidokeza kuwa hivi karibuni, Kiba alikuwa na shoo maalum mjini Arusha ambayo ilihudhuriwa na mamia ya wakazi wa jiji hilo ambapo siku hiyohiyo, Wema naye alikuwa na marafiki zake wakisherehekea na wenyeji wake, hivyo baada ya kuisha na kusikia Kiba yupo mjini hapo, akaona ni fursa nzuri ya kwenda kumuona.
“Wema alialikwa na rafiki yake mmoja hivi huku Arusha sasa baada ya sherehe yao kuisha na kuambiwa Kiba anaangusha shoo, akaona bora aibuke Triple A akamuone,” kilisema chanzo hicho.
NI KUMKOMOA DIAMOND?
Katika aya nyingine, chanzo hicho kilimwaga ubuyu kuwa, Wema aliamua kwenda kwenye shoo hiyo ya Kiba akiamini atamrusha roho zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye anadaiwa kuwa haziivi na Kiba.
“Nasikia Wema alitaka kwenda ukumbini ili ikiwezekana apige mapicha ya kumwaga na Ali Kiba ili yakivuja yamuumize Diamond,” kilisema chanzo hicho.
TEAM KIBA WAMZUIA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, baadhi ya wapambe wa Kiba (Team Kiba) waliposhtukia mchezo huo, walimzuia Wema getini ili asiweze kuonana naye.
“Wema alikuja majira ya saa 7:45 usiku akiwa na timu yake, kufika pale walitaka kuingia, lakini kwa hali aliyokuwa nayo wakakataa kumruhusu. “Walijua lazima angefanya kitu kwa Kiba, kitendo ambacho wao hawakupenda, hivyo mabaunsa wakafanya kazi yao vizuri.
“Kitendo cha kumkatalia kuingia kilisababisha kizaazaa hasa kutoka kwa wapambe wake. Ilitokea patashika nguo kuchanika kabla ya kukubali yaishe na kuondoka zao,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuvutiwa waya na kusomewa mashtaka, Wema alitiririka; “Ni kweli nilikuwa Arusha kwa shughuli zangu, nilifikia Mount Meru ambayo pia baadaye Kiba naye alifikia na tulionana, usiku kulikuwa na pati ya marafiki zangu, tukawa huko tulipomaliza tukaenda kwenye shoo ya Kiba.
“Kwa kweli sikumbuki chochote maana siku hiyo nilikuwa nimelewa sana, kwa hiyo nashindwa kusema kama unachosema nilikifanya au la, ila kesho yake niliambiwa kuwa tulikwenda kwenye shoo ya Kiba na hatukuingia.
“Hata wakati wa kurudi hotelini kwetu sikujua nilifikaje, zaidi ya kesho yake asubuhi niliwasikia kina Martin wakisema kwamba tulienda Triple A lakini kweli hatukuingia kutokana na fujo zilizokuwa zimejitokeza pale hivyo tukaamua kurudi kulala.”
Credit:GPL
4 comments:
yule doctor anayesema shilole atakuwa anaumwa na anahitaji psychologia basi mimi naona huyu bibiye wema sepetua madame anahitajia yeye sana huyu psychologist apimwe atafutiwe tiba na tiba nahisi ni mume anajishebedua tu but mume dawa apewe atuliye.
mtu analewa hata hajitambui uzungu gani huu,ugwana gani huu,ndo tuseme mtoto wa mjini,khaaa!! aibu na fedheha iliyoje. hivi mzee wake anaona raha kusikia mwanawe yupo hivi hivi kwa nini wasimtafutiye mume.
kuwalea watoto kizungu sana ndo matokeo yake haya ya UHAYAWANI NA UPUNGUWANI.KHAAAA!!!MWAFYUU!!!!!
AIBU MWENZANGU WEEE.NA ASAIDIWE JAMANI HUYU MADAME
Wema jamani tunakupenda ila tabia zako saa nyingine unatuboa ss kweli we utalewaje mpk usijitambue?pls ushauri mdogo tu acha kunywa pombe bwana.
Wema maradhi matatizo kuchanganyikiwa hajui atendalo yote ni kwa sababu ya dimondo asijitie bureeee kujifanya she doesnt care MUONGO HAJIWEZI mana haiwi mtoto wa kike kufanya mambo hata huyo mwanamme hayafanyi.
Mtakaaa mkimlaumu diamond but huyu wema ana matatizo sana nadhani diamond alimvumilia sana,mdau wa mwanzo kabisa nakubaliana na wewe kabisa huyu wema anahitaji psychologist something is wrong with her,she's acting so stupid,childish,
Post a Comment