ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, April 4, 2015

[AUDIO] Dakika 90 za dunia..Uchaguzi Nigeria

Bahati Alex wa Capital Radio Dar Es Salaam na Mubelwa Bandio wa Kwanza Production Washington DC
Wiki hii, historia imeandikwa kwenye siasa za Afrika. Nchi yenye watu wengi na uchumi mkubwa barani Afrika , Nigeria,  imeshuhudia mabadiliko ya uongozi ya amani kupitia sanduku la kura. Hii ni mara ya kwanza kwa jambo hilo kutokea tangu iondokane na utawala wa kijeshi mwaka 1999. Lakini pia, kuna mengi ambayo yamejitokea katika uchaguzi huo, na ambayo yanatazamwa sana kuelekea miaka minne ijayo.

Hii ni sehemu ya ripoti ya Kwanza Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii ilikuwa ripoti ya Aprili 4, 2015

No comments: