ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, April 4, 2015

SHUKURANI ZA DHATI

Kwa niaba ua Ben Mgawe, Tino na Mary Malinda na familia ya marehemu Eddis Mgawe, tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki mliojitolea kwa hali na mali kufanikisha safari ya mwisho ya baba yetu mpendwa Eddis Mgawe.
Hatuna cha kuwalipa lakini tunamuomba mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awajazie pale mlipopungukiwa na awape moyo wa kuzidi kushikamana kama waTanzania. Amen.

Mapato na matumizi ya michango ni kama ifuatavyo
pesa iliykusanywa ni $16, 692 (michango, harambee, VOA, Oklahoma na direct deposit kwenye account).
-Malipo ya awali ya funeral home $7252. Kwasababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu safari ya mzee wetu ilishindikana siku ya Ijumaa April /3/2015. Safari ya mzee wetu inafanyika siku ya siku ya Jumapili April/5/2015 na gharama tulizoongeza kwa funeral home ni $1759. 

Familia wao wameondoka Siku ya Jumamosi April 4/2015.

-Hivyo basi pesa iliyokwenda funeral home ni $9011. 
-Pesa ilyotumika kwa nauli ya wasafiri ni $6600. 
-Tulimshikisha kidogo kijana aliyetufaa kanisani $50. 
-Kwahiyo jumla ya matumizi ni $15661. Balance iliyobaki ni $1081 ambayo tumewapa familia iwasaidie wakifika Tanzania.
Asanteni Sana.
Kwa maelezo zaidi au ufafanuzi tafadhali wasiliana na mwenyekiti wa kamati Bwn Iddi Sandaly tel 301 613 5165

No comments: