Mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye atabeba jukumu la kupeperusha bendera ya chama hicho ili kukipa ushindi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, sasa tunahesabu siku.
Baadhi ya makada wa chama hicho wakiwemo wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), wanasema mchakato huo huenda ukaanza Mei mwaka huu.
Akizungumza na Mwandishi wetu, Mjumbe wa NEC kutoka mkoani Arusha ambaye hakutaka jina lake liandikwe, alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, CCM kitaandika historia ya kumteua mgombea urais mwenye vigezo vyote.
Alisema mgombea huyo ni yule ambaye atakidhi vigezo 13 ili aweze kukivusha chama hicho kiendelee kushika dola si kuteua mgombea anayetokana na shinikizo la makundi ya watu mbalimbali kama ilivyoanza kujionesha kwa baadhi ya wagombea wenye dhamira ya kuwania nafasi hiyo.
Mjumbe huyo alikwenda mbali zaidi na kusisitiza kuwa, chama hicho kina utaratibu mzuri wa kuchagua wagombea wake kwenye nafasi ya urais, ubunge na madiwani ambao ndio utazingatiwa katika kuwapata wagombea si vinginevyo.
"Chama kikichagua mgombea kwa sababu ya ushabiki na kelele za makundi ya watu kudai mwanachama fulani ndiye anayefaa kuwa rais na kutaka achukue fomu watamuunga mkono, nchi haitakuwa salama na sababu tunazo.
"Lazima tujiulize kwanini iwe yeye wakati kuna baadhi ya makada ndani ya CCM wanaotajwa kutaka kuwania urais wakiwa na sifa zinazokubalika ndani ya chama kuliko huyo wanayemtaka...chama hakiwezi kusikiliza maneno ya watu kwani nafasi yenyewe ni nyeti,"alisema.
Aliongeza kuwa, uteuzi wa mgombea urais CCM baada ya wagombea wote kuchukua fomu za kuomba kuwania nafasi hiyo, kila mmoja atatakiwa kutafuta wadhamini kwenye mikoa 10 na kuzirudisha kwa mchakato mwingine.
Majina ya wagombea hao yatapelekwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo itayapitia na baadaye kwenda Kamati Kuu kwa ajili ya uteuzi wa majina matano.
"Haya majina matano yatapelekwa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ili yaweze kupigiwa kura na kupatikana majina matatu ambayo yatapelekwa katika Mkutano Mkuu ambao nao utapiga kura ili kumpata mgombea mmoja," alisema.
Sifa za wagombea urais
Mjumbe huyo aliongeza kuwa, ili mgombea urais wa CCM aweze kuchaguliwa katika nafasi hiyo mbali ya kupitia taratibu alizozitaja awali ndani ya chama:
kwanza ; anapaswa kuwa na uwezo wa kuliongoza Taifa kwa kuzingatia uzoefu alionaokatika uongozi wa shughuli za Serikali, umma na taasisi.
Pili; awe mwadilifu, mwenye hekima na busara.
Tatu; awe na elimu ya kiwango cha Chuo Kikuu au inayolingana na hiyo.
nne; awe mwenye upeo na uwezo mkubwa wa kudumisha, kuimarisha na kuendeleza Muungano wetu, umoja, amani na utulivu wetu pamoja na mshikamano wa kitaifa.
Tano; awe mtu wa kuona mbali, asiyeyumbishwa, mwenye uwezo wa kufanya uamuzi wa busara kuhusu masuala nyeti na muhimu ya Taifa kwa wakati unaofaa.
sita; awe na upeo mkubwa usiotiliwa shaka kuhusu masuala ya kimataifaili aweze kuwa kiungo imara kati ya nchi yetu na Dunia yote kwa jumla.
Saba; asiwe mtu mwenye hulka ya udikteka au ufashisti bali aheshimu na kuilinda Katiba ya nchi, sheria, utawala bora, kanuni na taratibu za utawala bora.
nane; awe mtetezi wa wanyonge, kusimamia haki za binadamu, mzingatiaji makini wa maendeleo ya raia wote na asiwe na tamaa ya kujitafutia umaarufu wake binafsi.
Tisa; awe mstari wa mbele kuzifahamu, kuzieleza, kuzitetea na kuzitekeleza Sera za CCM na Ilani ya CCM ya Uchaguzi.
kumi; awe mpenda haki na jasiri wa kupambana na dhuluma,maovu yote nchini.
kumi na moja; asitumie nafasi yake ya uongozi kujilimbikizia mali.
Kumi na mbili; awe ni mtu anayekubalika na wananchi.
kumi na tatu; awe makini katika kuzingatia masuala ya uwajibikaji wa uongozi, watendaji, asiyevumilia uzembe katika utekelezaji wa majukumu ili kuinua nidhamu ya kazi, tija na ufanisi.
Aliongeza kuwa, kati ya sifa 13 za mgombea urais CCM zilizotajwa na Mjumbe wa NEC, kutokana na uchanga wanchi yetu, lazima mgombea awe na upeo mkubwa usioatiliwa shaka kuhusu masuala ya kimataifa ili aweze kuwa kiungo imara kati ya nchi yetu na Dunia yote kwa jumla.
3 comments:
Sounds good to me although am not a CCM fun.
Ante mdau mwandalizi wa hii habari nzito.!! mhh! Kwa kufupisha tu sidhani kama bado CCM wana MGOMBEA wa aina hii bado tunagubikwa saaaana, Nasema hivyo kwa nini? Zile mil. 306 za ESCROW zilizogagwa kinyemela na hadi leo hii hakuna aliyedhiriki kuzirejesha, hatuna imani na yeyote awaye!! Uchumi wa Tanzania umezidi kudidimia kutokana na fedha hiyo kutokuwepo kwenye mfumo!!Aliyetoa kakubali aliyepokea kakubali kwanini sharia isifanye kazi yake! MWALIMU ALILISEMA HILI LAKINI LEO TUMELIFUMBIA MACHO!! Niseme wazi tu mwandishi wa habari hii amelenga sana kwa mhe. Lowasa, Sita na Mwigilu KWA UFUPI WOTE HAWA HAWATUFAI KWA KUWA BADO NCHI ITAKWISHA!! NA PILI baadhi elimu ni ndogo!! Usiniulize!!
Tunachohitaji WaTanzania ni RAIS anayeweza kuwawajibisha waliochukua fedha za ESCROW wote wazirejeshe na kuhukumiwa, Raisi anayeweza kutetea maslahi ya WTanzania, Kuilinda fedha ya Tanzania na mfumuko wa bei kila siku ili mTanzania wa kawaida aweze kuishi na kupeleka mtoto shuleni, kwani elimu ndio kinga ya maisha ya baadae. Raids anayeweza kuboresha miundo mbinu kwa maana ya barabara zetu kupunguza ajali. Mwisho hospitali zetu ziwe bora. Bila kusahau kukusanya kodi ipasavyo na swala la RUSHWA likomeshwe watu wajifunze kutoa huduma bila rushwa. Katiba yetu iwe na maslahi kwa wananchi na sio CCM ambayo kesho haitakuwepo.. Asante wadau.
Kwa maelezo haya imejionesha dhahir kama hata kikwete nae hajuwi amchaguwe nani kati ya PINDA na SITA ambao ni watu hawawakubali kwa ubabe wao na hii sio siasa nzuri mgeliona mbali ni afazali Mwingulu Nchembe ambaye bado hana matokeo ya ajabu ajabu kuliko kulazimisha mgombea aliejaa ubaya midomoni mwa watu
Post a Comment