Advertisements

Monday, April 13, 2015

HAWA NDIO WASANII WATAKAOGOMBEA UBUNGE KUPITIA CHADEMA


Hii tabia ya CHADEMA kutumia wasanii wa bongo fleva & movie kisiasa ni upunguani wa hali ya juu sana.
Iweje leo hii kisa tu chama kinataka ruzuku ya kutosha kione ni vyema na sawa kuokota tu vijana wasio kuwa na maadili kutoka kwenye tasnia za muziki na movie na kuwanadi ili wawakilishe wananchi bungeni!? Huu ni wehu na kukosa kufikiri!

CHADEMA wamezindua mpango uitwao "Kujaa bungeni kivyovyote" na haya ya kujaza wasanii ndio mkakati wa kufanikisha mpango huo!

Kwa taarifa sahihi kutoka CHADEMA makao makuu, wafuatao wanatarajiwa kusimamishwa na CHADEMA kwenye majimbo ya uchaguzi oct mwaka huu:

1) Irine Uwoya - Jimbo la Mtera

2) Prof Jay - Jimbo la Mikumi

3) JB (bongo movie) - jimbo la Kigamboni

4) Sugu - Jimbo la Mbeya Mjini

5) Juma Nature - Jimbo la Temeke

6) Dully Sykes - Jimbo la Ilala

7) Fid Q - Jimbo la Magu


Je, wewe Mtanzania una kubaliana na hawa CHADEMA kukupa wawakilishi wa aina hii? Maana CUF na NCCR hawana kauli huku bara ya kupanga wagombea wanaojitambua na kujua wajibu wao kwa wananchi.

3 comments:

Anonymous said...

Wewe inakuhusu nini wakigombea wasanii? Mbona CCM wanatumia vihiyo wengi wasio na elimu na wengine mafundi vyerehani. Si nafuu wasanii ambao wengi ni vioo katika jamii kuliko mafisadi wa CCM wanaoendelea kutufanya tuendelee kuwa maskini?

Anonymous said...

Two wrong does not make one right.Nadhani wakati umefika Tanzania ipitie upya qualifications za wagombea ubunge.Mbunge ni mtungaji wa sharia sasa tuweke itikadi za vyama pembeni, fundi cherehani, nganga wa kienyeji,mbongo fleva asiekuwa na collage qualifications au mtu yoyote ambae hajahitimu walau a diploma in something kakweli niseme "yatosha sasa".Tumechoka kuwa na wabunge wagonga meza.Zuri,Baya,lisilo sahihi wanagonga meza kwa umbumbu wao.

Anonymous said...

BUT HII HABARI SIDHANI KAMA IPO SAHIHI NA PIA IMEKAA KAMA YA UPANDE MMOJA YENYE NIA YA KUCHAFUA UPANDE MWINGINE NA PIA MWANDISHI AMEKOSA WEREDI WA KUWA HURU KATIKA KUFIKISHA HABARI