ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 17, 2015

LULU AFUTA AKAUNTI YAKE YA INSTAGRAM KUFUATIA KIFO CHA MTU ALIYEDAIWA KUWA MPENZI WAKE

 Muigizaji wa filamu, Elizabeth ‘Lulu’ Michael mwenye wafuasi wengi kwenye Instagram, ameamua kujiondoa baada ya kushambuliwa kwa matusi na baadhi ya watu kufuatia kifo cha mtu aliyewahi kuwa mpenzi wake.

Kufuatia kifo cha kutatanisha cha Lusekelo Samson Mwandenga ‘Secky’, watu wengi walianza kumtukana Lulu wakimhusisha pia na kifo hicho huku pia wakipost picha zinazomuonesha alipokuwa na marehemu.
Hata hivyo mujibu wa Global Publishers, familia ya Secky imeweka wazi chanzo halisi cha kifo chake.
Familia hiyo imeeleza kuwa marehemu aliumizwa na kiti cha kioo akiwa kambeba mtoto wake nyumbani kwake kisha akapelekwa hospitali na baadaye kufariki dunia akiwa huko.
Katika hatua nyingine msanii mkongwe wa filamu, William Mtitu amefunguka na kuwataka watu kuacha kumshambulia Lulu kwa kitu ambacho hahusiki nacho.

“Lulu ni msanii mdogo sana kiumri na amepitia mitihani mikubwa sana katika maisha ambayo mimi na wewe kabda tusingeiweza kuikabili plz nawaomba tumuache kwa sasa inatosha jamani kumbukeni huyu ni binadamu na moyo kama nilivyokuwa mimi na wewe hivi utajisikiaje km utasikia lulu amejizulu kwa namna yeyote ile kutokana na maneno yako ya kumshambulia mitandaoni,” ameandika kwenye Instagram.
“Kumbukeni sisi ni banadamu atuijui leo yetu itaishaje wala kesho yetu itakuwaje? Plz inatosha sasa watanzania wenzangu. MTAARIFU NA MWINGINE.”
Miaka miwili iliyopita Lulu aliwahi kukaa jela kutokana na kushtakiwa kwa kumuua bila kukusudia Steven Kanumba aliyekuwa mpenzi wake.

CHANZO: BONGO 5

No comments: