ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 19, 2015

Mahojiano na Linda Bezuidenhout (LB) Pt I

Karibu katika sehemu ya kwanza ya mahojiano na mbunifu wa kimataifa wa mitindo mwenye asili ya Tanzania, Linda Bezuidenhout.
Ameeleza mengi ikiwa ni pamoja na historia yake kwa ufupi, safari yake kwenda nje ya nchi, alivyorejea na kuanza harakati zake za mitindo.
Nani alimfanya ashawishike na fani hii?
Maisha yake kimahusiano je?
Familia yake sasa na inavyokabiliana na kazi zake?
KARIBU

instagram ya Linda ni lb_apparel na Facebook Linda Bezuidenhout apparel 
makeup by Candice Gibson

6 comments:

Anonymous said...

Binafsi yangu nakukubali sana katika shughuli zako ! Safi sana !nimesikiliza mahojiano yako ! Ulipotaja shule ya msingi uliyosoma nikakukumbuka vizuri sana kwani tulisoma wote pale Mbuyuni ! Nikawakumbuka na wanafunzi wengine tulio soma wote kina , Mganyizi Mwijage, Sandra Mushi, Mzomu Banyikwa-R.I.P, Standi bichwa na dada zake! Allan Magesa, Charles Shengena, Kalunde Kasiga, Amina Mwalimu-R.I.P, Isabela Buzuwili , Muli Mkinga ,Gwantwa Mkinga!Omari Mzirai na wengine wengi tu! Nakutakia mafanikio zaidi katika shuguli zako walau siku moja LB iwe juu sana ! Mimi nakuita wewe ni Jasili kwa lugha anayotumia Kalapina !

Anonymous said...

Dah umenikumbusha sana enzi za Mbuyuni ulivotaja hao wanafunzi kina Sakina Pamela RIP, Fatuma RIP nilikuwa sijui Amina Mwalimu kashatangulia, R.I.P Amina. dada zake stand ni Peshe na Frola. Eti Standi Bichwa umenichekeshaaaaa ha ha haaaa. Sera Ishengoma rafiki yangu facebook uwa ananiwekea comments nzuri sana za kunisupport, Charles Shengena alikuwa ndo Genius wetu alikuwa na akiriiiii yani umenikumbusha mbali my dear Shukran sana usikose part 2. Mimi ni Linda.

Anonymous said...

looking good bidada kama kawaida.
interview nzuri, good location.
mjasiriamali mwenzako in DC

Anonymous said...

Nimependa sana hii interview, inafurahisha kuona watanzania wenzetu wa majuu mnavyowakilisha vipaji vyenu, hongera sana kwa kuweza kufanikisha talent zako katika nchi za kigeni, kuna vipaji vingine kibongo vinaonekana ni vya kawaida lakini majuu ni vipaji muhimu sana, huwa natembelea page yako nadmire sana kazi zako,naisubiri kwa hamu part 2, endelea na moyo wa kushare ideas mbalimbali na sisi wabunifu wachanga ambao tunatafuta jinsi ya kuonyesha vipaji vyetu, nimejifunza mengi sana kwenye hii interview, mungu akubariki wewe na familia yako

Anonymous said...

Linda nakupendaga mie acha tu, mwanamke unafit kila depatrment, mzuri, hardwork, unajua kuparty, kuishi big, familia bora, watoto wazuri mungu akulinde na akuongezee kila ufanyalo

Anonymous said...

Hilo location la mahojiano ni wapi bandugu? duhh vikwangua anga hapo kwa nyuma ni hataree