ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 30, 2015

MBUNGE WA MVOMERO AINGILIA KATI MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUHUSIANA NA BONDE LA MGONGOLA

Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla akimpa pole na fedha za matibabu mmoja wa wakulima aliyejeruhiwa kwa kuvunjwa Mkono. 
Maelfu ya wananchi wakimsikiliza kwa makini baada ya Mbunge wao Amos Makalla kukubali kufadhili Kamati ya kwenda kumuona Waziri mkuu.
Mamia ya wananchi akimpokea mbunge wao aongee na wakulima bonde la Mgongolwa.


Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla akiongea na wananchi nje ya kituo cha polisi kuwa mahabusu wapo salama
Mbunge wa Mvomero, mkuu wa wilaya , Kamati ya ulinzi na usalama na wenyeviti wa Vijiji wakiwa kituo cha polisi Dakawa kuwaona mahabusu wanaoshikiliwa polisi kufuatia machafuko ya wakulima na wafugaji watu 3 wamekufa.



Mbunge wa Mvomero Mh, Amos Makalla ameridhia pendekezo la wananchi kumuona Waziri Mkuu Mh, Mizengo Pinda kufuatia mapigano ya wakulima na wafugaji yaliyotokea wiki iliyopita ambapo watu watatu walipoteza maisha huku wengine wengi wakijeruhiwa baada ya wafugaji kulishia Mazao ya wakulima katika mashamba yaliopo bonde la mgongola.


Kutokana na hali hiyo, Mbunge huyo kwa kushirikiana na Mkuu wa wilaya na kamati ya ulinzi na usalama waliitisha mkutano wa hadhara kijiji cha Kugugu kuongea na wakulima wanaolima katika bonde la Mgongola, ambapo pamoja na mambo mengine wananchi walimuomba Mbunge wao kuundwe Kamati ya kumuona Waziri mkuu Mizengo Pinda kuhusiana na mipaka ya bonde la Mgongola ambalo limekuwa mahakamani kwa zaidi ya miaka 15 na machafuko ya mara kwa mara yametokana na bonde hili kwa wafugaji wa kijiji cha Kambala kulishia mifugo Mazao ya wakulima na kupelekea uvunjifu wa Amani wa mara kwa mara.


Akiongea kwa niaba ya wananchi, mkazi wa Kigugu ndugu Salihina Mpenda alisema kuwa "kesi ya bonde la Mngongola imekuwa muda mrefu na serikali haichukui hatua huku watu wanaendelea kufa kila kukicha, na imefika wakati jitihada zako Mbunge ulizozifanya kuwaleta mawaziri 4, barua ulizomuandikia Waziri mkuu na Waziri wa ardhi sisi wananchi tunakupongeza ila inapaswa tukuongezee nguvu tukamuone Waziri mkuu" alisema mkulima huyo.


Akijibu hoja hiyo, Mbunge na Naibu Waziri aliridhia ombi lao la kuundwa Kamati ya wakulima ya kumuona Waziri mkuu na akawataka wachague watu kumi na yeye kama Mbunge atagharamia gharama zote.

Aidha kwa upande mwingine mkuu wa wilaya hiyo Festo Kiswaga amewahakikishia hali ya usalama ndani ya bonde la Mgongola ni shwari wakulima waendelee na shughuli zao kwani na Ulinzi wa Askari wa doria umeimarishwa.

No comments: