Kuna siku nilihudhuria harusi moja kanisani na kitu kimoja kilinishangaza na kunifanya niwe na maswali mengi yasiyokua na majibu.
Siku hiyo Bwana harusi mtarajiwa aliwahi kanisani kama kawaida akiwemo bi harusi mtarajiwa nae alifika kanisani kwa muda unaotakiwa lakini gari lililomleta lilitakiwa kufuata watu wengine kwa ajili ya na kuwaleta kanisani na kwa maana hiyo harusi ndoa ingeweza fungwishwa mpaka watu hao wafike.
Bi. harusi mtarajiwa aliambiwa aningie ndani kanisani lakini aende nyuma ya kanisa kusubili mpaka hapo atakapoletwa mbele kwa ajili ya ndoa.
Wakati huo Bwana harusi na wapambe wake walikua tayari wapo ndani ya kanisa wakisubili taratibu za harusi zifanyike zikiwemo za kuletwa na mzazi wake kumkabidhisha tayari kwa tendo la kufunga ndoa lifanyike.
Kilichonishangaza ni pale niliposikia mmoja ywa waandaji wa harusi akimweleza Bwna harusi mtarajiwa na wapambe wake wageuke wasimwangalie bi. harusi mtarajia anapoingia kanisani kwani ni nuksi kumwona bi harusi kabla ya ndoa hii inaweza fanya ndoa isidumu. Nikaanza kujiuliza maswali mengi ikiwemo la Bi. harusi kuficha uso wake mpaka baada ya ndoa ikishafungwa ndio hufunua uso wao lakini ukweli wa hili swala silijui undani wake je kuna mtu yeyote mwenye ufahamu na swala hili.
No comments:
Post a Comment