Mwanachuo Milicent Murugi akiongeaa na wanahabari Picha na Jeff Angote
Mwananfunzi mmoja Milicent Murungi wa chuo kikuu cha Garissa ambaye ni mjamzito wa miezi 8 amesema ilibidi ajifanye amekufa chuo chao kilipovamiwa na wapiganaji wa Al shabab na kuua wanachuo wasiokua na hatia.
Milicent Murungi akiongea na waandishi wa habari alisema ilibidi ajifanye amekufa kwa saa 10 baada ya wenzake waliokua nao kwenye chumba hicho kuawa na yeye kuchukua damu ya mmoja ya wanafunzi kujipaka kichwani wakati huo wapiganaji hao wa Al Shabaab walisikika wakielekea vyumba vya juu na kmbakiza mmoja pale chini alipokuwepo.
Milicent Murungi kutoka Embu na mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho cha Garissa alisema taratibu alichukua damu na mwanachuo mwenzake aliyekua amekufa jirani yake na kujipaka kichwani na kujifanya amekufa kwa saa 10.
No comments:
Post a Comment