ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 5, 2015

MWIMBA INJILI REBBECA MALOPE ATUA DAR, KUINOGESHA SIKUKUU YA PASAKA LEO

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama akiupokea ugeni wa Mwimbaji wa Muziki wa Injili kutoka nchini Afrika Kusini, Rebbeca Malope baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar.
Mwakilishi wa Msama Promotion, Nyakwesi Mujaya akimvisha skafu Mwimbaji wa Muziki wa Injili kutoka nchini Afrika Kusini, Rebbeca Malope mara alipotua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana.
Mwakilishi wa Msama Promotion, Grace Khuni akimkabidhi ua Rebecca mara baada ya kuwasili Dar.
Rebbeca Malope akipunga mkono kwa mashabiki (hawapo pichani) akiwa na mwenyeji wake ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama (kulia) baada ya kuwasili kwenye jijini Dar jana jioni tayari kwa kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka linalofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar, ambapo Solly Mahlangu mwanamuziki nguli mwingine wa muziki wa injili kutoka nchini humo atawasili leo na kujiunga moja kwa moja na tamasha hilo kushoto ni Mume wa Rebbeca.
Rebbeca Malope akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuwasili Dar.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jana jioni mara baada ya kumpokea Rebbeca Malope.
Rebbeca Malope, akifurahia skafu aliyovishwa na mmoja wa wawakilishi wa Msama Promotion, Nyakwesi Mujaya.
Rebbeca Malope akiwa amepozi katika picha na Mwandishi wa Azam TV, Timzoo Kalugira.
Rebbeca Malope katika picha na wawakilishi wa Msama Promotion kushoto ni Nyakwesi Mujaya na kulia ni Grace Khuni.
Rebbeca Malope katika picha na wawakilishi wa Msama Promotion wa pili kushoto ni Nyakwesi Mujaya, kulia ni Grace Khuni na wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa Maandalizi ya Kamati ya Pasaka, John Melele.
Rebbeca Malope, akiimba kwa furaha na akisema amefurahi kufika Tanzania na anaipenda Tanzania.

No comments: