Msimamizi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Msimbazi Centre kilichopo jijini Dar es Salaam, Sister Anna Marandu (kulia) akipokea msaada wa chakula na vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaolelewa kituoni hapo kutoka kwa Meneja wa benki ya CBA tawi la barabara ya Nyerere, Nuru Mwangulangu wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipotembelea kituo hicho kutoa misaada mbalimbali na kucheza na watoto leo ikiwa ni moja ya shamrashamra za kkuwapa burudani katika kipindi hiki cha Sikuu ya Pasaka. Wengine pichani ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto Yatima cha Msimbazi wakifurahia zawadi mbalimbali zilizotolewa kwa ajili yao na benki ya CBA, waliosimama ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo ambao wametembelea kituo hicho kwa ajili ya kutoa zawadi mbalimbali na kucheza na watoto ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Sikukuu ya Pasaka.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya CBA wakiwa katika picha ya pamoja na Msimamizi wa Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Msimbazi kilichopo jijini Dar es Salaam, Sr. Anna Marandu na baadhi ya watoto wanaolelewa kituoni hapo muda mfupi baada ya kukabidhi msaada wa chakula na vitu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia watoto hao leo ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Sikukuu ya Pasaka.
BENKI ya Commercial Bank of Africa (CBA) leo imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo cha Msimbazi kilichopo Ilala jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wafanyakazi hao walishiriki kulea na kucheza na watoto hao ikiwa ni njia ya kuwaonyesha upendo.
Akizungumza kituoni hapo Meneja wa benki hiyo wa tawi la Nyerere ,Nuru Mwangulangu,ambaye aliongoza wafanyakazi wenzake waliofika kituoni hapo alisema wamefanya hivyo kama sehemu ya utaratibu wao wa kuchangia makundi yenye mahitaji maalumu kwenye jamii hususani watoto ambao ndio tunaamini wanapaswa kuandaliwa vizuri na kupata mahitaji muhimu na haki wanazostahili kwa kuwa ndio taifa la kesho.
“CBA leo tumekuja kuwaona vijana, kufurahi nao,na kuwapatia zawadi ili kuwawezesha kufurahia sikukuu ya Pasaka kama watoto wengine waliopo majumbani.watoto kama hawa wanahitaji upendo,faraja na kupatiwa misaada mbalimbali ya kuwawezesha kujisikia kuwa nao ni sehemu ya jamii na kusaidia jamii ni sehemu ya sera yetu ndio maana tumekuwa tukisaidia jamii katika Nyanja mbalimbali hususani elimu na afya”.Alisema Mwangulangu.
Pia alisema kufika kwao wameweza kuangalia mazingira, kufahamu changamoto zinazowakabili walezi wa kituo hicho na kuona wapi benki inaweza kusaidia katika siku za usoni na aliwataka wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia kutoa msaada na kutumia muda wao kusaidia makundi mbalimbali yenye mahitaji kwenye jamii.
Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa kituo hicho,Sista Ana Marandu,aliwashukuru wafanyanyakazi wa benki hiyo kwa kutoa msaada wa chakula ,nguo,kuwafungia watoto michezo ya burudani na kutumia muda wao kucheza nao. “Tunatoa shukrani kwa upendo mkubwa mlioonyesha siku hii ya leo na tunawaomba siku zote mtupe ushirikiano kama huu”.Alisema Sista Marandu
No comments:
Post a Comment