CMB Prezzo.
MAPEMA mwaka jana, rapa wa nchini Kenya, CMB Prezzo katika mahojiano yake redioni alisema atakuwa akiwania nafasi ya kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao.
Mbali na kuwa alisema siku moja atawania nafasi ya urais, baadhi ya vyanzo vya habari vimeeleza kuwa kwa sasa staa huyo anajiandaa kuzindua kampeni yake ya kuingia kwenye siasa.
Prezzo mwenyewe amethibitisha taarifa hizo kwa kusema: "Ni kweli nina mpango wa kuingia kwenye siasa"
"Kwa sasa bado nashauriana na washauri wangu wa kisiasa na nikiwa tayari na kujua ni nafasi gani niwanie, nitaujulisha umma", alisema mwanamuziki huyo.
CREDIT:GPL
No comments:
Post a Comment