Bondia wa ngumi za kulipwa, Mohammed Matumla.
IMEFAHAMIKA kuwa ile safari ya bondia wa ngumi za kulipwa, Mohammed Matumla kwenda kuzichapa katika pambano la utangulizi litakalowakutanisha mabondia Floyd Mayweather Jr dhidi ya Manny Pacquiao nchini Marekani, Mei 2, mwaka huu,
inaweza kuwa imeishia kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar.
Matumla alipata nafasi hiyo baada ya kumchapa kwa pointi Wang Xin Hua wa China katika pambano la Ubingwa wa Dunia wa WBF ambapo ilielezwa mshindi atasafiri mpaka Marekani kwa ajii ya pambano hilo.Taarifa za uhakika ni kuwa ratiba ya mabondia watakaopanda ulingoni siku hiyo imeshatolewa bila ya kuwepo kwa jina la Mtanzania huyo.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mohammed alisema: “Sioni kama kuna dalili za kwenda kupigana huko Marekani kwa sababu promota amekuwa haeleweki na kila ninapofanya mawasiliano naye anasema wanasubiria majibu ya video walizotuma napigana na Mchina.
“Makubaliano hayakuwa hivyo kwani wao walisema mshindi atakwenda Marekani, hata maandalizi bado sijaanza, unadhani kuna nini hapo?”Juzi, promota aliyesimamia pambano la Mohammed, Jay Msangi alipotafutwa alisema: “Niko bize naongea kwenye Skype na Rais wa WBF, Howard Golgberd kuhusu ripoti ya Mommed Matumla ambapo atakuwa na majibu, nitafute kesho (jana).” Alipotafutwa jana Alhamisi hakupokea simu.
No comments:
Post a Comment