ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 30, 2015

Tazama sehemu ya pili ya kipindi cha ‘UBISHI’


Katika mwendelezo wa kipindi cha ‘Ubishi - Komaa Upate Pesa’, wiki hii Bwana Costantine Magavilla anakuletea sehemu ya pili iitwayo ‘Kazi ni Tabia’. Kazi ni gumzo kwa vijana wengi wa mjini ila ni kitu gani kinacho wachochea vijana kufanya kazi haswa na je madhara yake ni nini kwao. Pata majibu kwa kutembelea www.magavilla.com

Usikose kufuatilia vipindi hivi vinavyolenga kuelimisha, kukuhamasisha utazame upya maisha yako upateujasiri wa kubadili fikra na kufanya yako kila wiki siku ya Jumanne.

Bwana Costantine Magavilla ni mwandishi wa kitabu kiitwacho 'Life and You' na ni mhamasishaji maarufu Tanzania katika makongamano mbalimbali kuhusiana na maendeleo binafsi na mabadiliko ya kibiashara. Ni mdau mkubwa wa masuala ya masoko hususan katika kutangaza biashara na miongoni mwa kazi zake ni kuwahamasisha vijana kujituma na kuchangamkia fursa.

Mwisho wa taarifa.

Imetolewa na Mancom Limited kwa mawasiliano zaidi tuandikie kupitia info@mancom.co.tz au costantine@magavilla.com

2 comments:

Anonymous said...

Hauleweki lugha yako unayotumia,unapotaka kuwaelimisha vijana tumia lugha rahisi inayokwenda na wakati(B) unapozungumza kama unatoa lecture Universty vijana wa kitaa na maisha kawaida hawezi kukuelewa,labda fungua kanisa

Anonymous said...

namuunga mkono mdau wa mwanzo jamaa anaelekea ni msomi ndo maana ana sema kama lectural lakini kwa kijana/vijana wa kitaa lugha aliyotumia hawatomuelewa japo kuwa ana point nzuri.

tujifunze kusema katika majukwaa na kila msikilizaji aweze kunufaika.