Mafundi wakiendelea na
kazi za ujenzi wa daraja kubwa la Kolo lenye urefu wa mita 60 katika barabara
ya Dodoma-Babati sehemu ya kipande cha barabara ya kutoka Mela kwenda Bonga
chenye urefu wa km 88.8. Ujenzi wa daraja hilo unatarajiwa kukamilika mwezi Mei
mwaka huu.
Meneja wa Wakala wa
Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dodoma, Eng. Leonard Chimagu (watatu kutoka kushoto)
akiwa na wahandisi wa barabara ya kutoka Mela-Bonga mara baada ya ukaguzi wa
daraja la Kolo.
Mafundi wakisuka nondo
kwa ajili ya kumalizia kalavati la duara katika barabara ya Dodoma (Mayamaya)
hadi Babati (Bonga) katika sehemu ya Mela kwenda Bonga km 88.8.
Mhandisi mshauri
katika barabara ya Mayamaya-Mela km 99.35
Eng. Godfrey Kombe akizungumza kuhusu maendeleo ya mradi wa barabara
hiyo uliofikia asilimia 18.
Kazi za ujenzi
zikiendelea kwenye tuta la barabara ya Mayamaya-Mela km 99.35.
Kazi za ujenzi
zikiendelea kwenye tuta la barabara ya Mayamaya-Mela km 99.35.
Fundi akichomelea
vyuma katika sehemu litakapojengwa boksi kalavati.
Katapila likichonga
barabara ya Mayamaya-Mela km 99.35.
Boksi kalavati likiwa
limekamilika katika barabara ya Mayamaya-Mela km 99.35.(Picha zote kwa Hisani
ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU)-Wizara ya Ujenzi)
Ujenzi wa Barabara ya Dodoma
(Mayamaya) hadi Babati km 188.15 katika sehemu ya Mayamaya-Mela km 99.35
pamoja na kipande cha Mela Bonga km 88.8 unaendelea vizuri na unatarajiwa
kukamilika mwaka 2017.
Kauli hiyo ilitolewa
na Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoani Dodoma Eng. Leonard Chimagu wakati
akifanya ukaguzi wa ujenzi wa barabara hiyo inayojulikana kama barabara kuu ya
Kaskazini iliyoanzia Cape town
nchini Afrika Kusini hadi Cairo nchini
Misri
“Katika barabara kuu
hiyo sehemu yetu ya Tanzania ndio ilikua haina lami ila kwasasa ujenzi umeanza
na unaendelea vizuri, ujenzi wa barabara katika sehemu ya kwanza ya
Mayamaya-Mela km 99.35 umefikia asilimia
18 na ule wa Mela Bonga km 88.8 umefikia asilimia 20 ya ujenzi wake” alisema
Eng. Chimagu.
Eng. Chimagu aliongeza
kuwa mkandarasi yupo katika hatua za
mwanzo na anaendelea vizuri na kama
hakutakuwa na vikwazo vyovyote basi ataikamilisha barabara hiyo kwa wakati”,
alisema Eng. Chimagu.
Kwa upande wa Mhandisi
Mshauri katika sehemu ya barabara ya Mayamaya-Mela km 99.35 Eng. Godfrey Kombe alisema kuwa kazi za
ujenzi zinaendelea vizuri na tayari mkandarasi ameshasafisha eneo la barabara
lenye urefu wa km 70.
“Tayari Mkandarasi
ameshasafisha eneo la barabara lenye urefu wa km 70 kwa kuondoa miti mikubwa,
pia ameweza kujenga jumla ya makalavati 52 ya duara pamoja na 12 ya boksi”,
alibainisha Eng. Kombe.
Aidha, Eng. Kombe
amesema kuwa ujenzi huo unahusisha pia ujenzi wa madaraja makubwa manne moja
likiwa na urefu wa mita 200 na mengine yakiwa na urefu wa mita 45 pamoja na
mita 30 madaraja mawili.
Kwa upande wa ujenzi
wa sehemu ya barabara ya Mela-Bonga km 88.8 Eng. Chimagu amesema kuwa
unaendelea vizuri na ujenzi wa daraja kubwa la Kolo lenye urefu wa mita 60 unatarajiwa kukamilika
mwezi mei mwaka huu.
Aidha, Mhandisi Mshauri
wa kipande hicho cha barabara ya Mela-Bonga- km 88.8, Eng. Kini Kuyonza alisema kuwa mkandarasi wa
barabara hiyo amefikia hatua nzuri kwa asilimia 20 na ujenzi unaendelea kama
walivyopanga.
Mradi huo wa ujenzi wa
Barabara ya Dodoma (Mayamaya) hadi Babati (Bonga) yenye urefu wa Km 188.15
unagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 183.
Imetolewa na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini (GCU)-Wizara ya Ujenzi
No comments:
Post a Comment