Balozi Henry Mdimu akiongea na vyombo vya habari
Taasisi isiyo ya ki serikali ya Imetosha Foundation inayopinga unyanyapaa, ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino kwa njia ya elimu, inatarajia kutuma ujumbe mzito kanda ya ziwa hapo kesho kwa maandalizi ya ujio wa timu nzima ya taasisi hiyo iliyojikita kwenye kubadilisha mtazamo (mind set) wa watu juu ya janga hili. Ujumbe huo utaongozwa na mwenyekiti wa taasisi hiyo Bw Masoud Kipanya, Balozi Henry Mdimu Mgaya na katibu Salome Gregory,wajumbe watakaongozana na viongozi hao ni pamoja na Mkala Fundikira, Isaya Mwakilasa (wakuvwanga aka Baba Andunje) Zaytun Biboze, Kelvina John na msanii wa muziki wa reggae Jhikoman Manyika.
Mwenyekiti Masoud Kipanya akiongea katika kilele cha matembezi ya hamasa yaliyofanyika jijini Dar.
Dhumuni la safari hiyo itakayoupeleka ujumbe huo mpaka mkoani Shinyanga ni kwenda kujitambulisha kwa viongozi wa serikali na usalama wa mikoa na za kanda hiyo iliyoathiriwa sana na janga la ukatili na mauaji ya watu wenye ualbino. Taasisi ya Imetosha imepanga kwenda kanda ya ziwa baadaye mwezi ujao ambapo timu itaenda maeneo yaliyoathiriwa na kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo hayo kuwa si kweli kwamba ukiwa na kiungo cha mtu mwenye ualbino utapata mafanikio, elimu hizo zitatolewa kwa njia ya filamu mbali mbali, michezo ya kuigiza na matamasha ya muziki.
Hoteli ya Green Palm utakapofikia ujumbe wa Imetosha Foundation jijini Mwanza aka the Rock City. |
Isaya Mwakilasa wa (Orijino komedi) Henry Mdimu na familia ya Isaya aka Wakuvwanga |
Maktaba Baadhi ya wajumbe wa Imetosha wakijiandaa kwenda katika mchezo wa Simba na Yanga |
No comments:
Post a Comment