ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 17, 2015

KIJANA DAUDI MRINDOKO MGOMBEA MWENYE UMRI MDOGO ZAIDI KILIMANJARO

Moshi,Kilimanjaro,
Wakati tunahesabu miezi kuelekea uchaguzi mkuu 2015,mengi ya kufurahisha yanahibuka kama vile wananchi wa jimbo la Moshi Mjini kumshawishi mgombea waokijana Daudi Babu Mrindoko achukue fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo 2015,na kumiminia sifa zote zinazofaa kijana huyo wa mjini Moshi achaguliwe.wakazi hao wa jimbo la Moshi Mjini kwa sasa wanadai kuwa kijana wao waliomshawishi achukue fomu ndiye Mgombea kijana mwenye umri mdogo kuliko wengine wote wenye nia ya kugombea ubunge mkoani Kilimanjaro,kwani Daudi Mrindoko ana umri wa miaka 30 tu, na hakuna wa mgombea yoyote hadi sasa mwenye umri chini ya miaka 30 mkoani Kilimanjaro. Wenyewe wakazi wa jimbo la Moshi mjini wanadai kuwa kijana huyo mdogo ndio pendekezo na tumaini lao la uchaguzi 2015,na wanahidi kumpa kila wawezalo bila kujali atagombea kwa kupitia tiketi ya chama gani,wanachojali uwezo wake wa kuwatumikia na kuwawakilisha bungeni.
Kijana Daudi Babu Mrindoko(30) ni mkazi wa Moshi mjini,Mjumbe wa UVCCM mkoa Kilimanjaro,pia mwenyekiti wa tahasisi ya Umoja wa wazalendo Tanzania(UWATA) inasemekena ni kijana mwenye mvuto sana kwa jamii kutokana na ukaribu huo wananchi wa jimbo la Moshi mjini uwambii chochote juu ya kijana wao huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye wamempa majina mengi
kama a.k.a Obama wa Moshi, na kauli mbiu ya ni "Moshi Panafukuta Moto 2015' Pendekezo hilo la wana Moshi mjini pia linapatikana at www.facebook.com/mrindoko.mwidadi



No comments: