Mwana-daispora Walter anayeishi katika jiji la San Francisco - California akitoa maelezo mafupi kwa mweshimiwa raisi wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete kuhusu shughuli za organization yao (Powering Potential). Mdau Walter ni mwanadiaspora yuko Tanzania kuhudhuria Tamasha la Elimu lilofanyika mjini Dodoma kuanzia tarehe 11-15 May 2015.
Mwana-diaspora Walter akiendelea kumwelekeza mheshimiwa raisi Jakaya Kikwete jinsi gani tekinolojia ya kompyuta ambayo inatumiwa mionzi ya jua
inavyofanya kazi na kutumiwa vyema na wanafunzi wa sekondari walioko vijijni.
Mheshimiwa raisi Jakaya Kikwete akionyesha alama ya dola gumba kufurahishwa na
tekinolojia hiyo ya kompyuta inayotumia umeme wa jua katika shule za sekondari vijijini Tanzania. Mwana-daispora Walter amefarijika sana kuona kuwa raisi wake amedhamini tekinolojia hio na kuona mchango wa mwana-diaspora huyo katika suala zima la kusaidia nchi katika suala zito la elimu. Maelezo zaidi kuhusu tekinolojia hiyo tumia barua pepe walterminja@poweringpotential.org