ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 16, 2015

Lowassa afunika Arusha

Arusha. Shughuli mbalimbali jijini Arusha jana zilisimama kwa muda wakati umati wa watu ulipofurika kumlaki Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyewasili mkoani hapa kwa ajili ya kuendesha harambee ya ujenzi wa Msikiti wa Patandi ulioko wilayani Arumeru.
Lowassa, ambaye jana aliweka bayana kuwa atatangaza rasmi nia yake ya kuwania urais kwa tiketi ya CCM, alienda kuendesha harambee kwenye msikiti huo baada ya kutumwa kumwakilisha Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal.
Katika shughuli hiyo ya harambee, Lowassa alifanikiwa kuchangisha Sh235 milioni, ikiwa ni zaidi ya makisio ya msikiti huo ya kukusanya Sh200 milioni.
Harambee zimekuwa zikichukuliwa kama uwanja wa kampeni wa makada wanaowania urais kupitia chama tawala cha CCM na tangu apewe adhabu na wanachama wengine watano, Lowassa hakuwahi kuonekana kwenye uchangishaji fedha hadi wiki mbili zilizopita alipoalikwa na wagombea wengine wa urais wa CCM kwenye hafla iliyofanyika Zanzibar.
Jana, mbunge huyo wa Monduli alipokelewa kwa mbwembwe kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha ambako alilakiwa na umati wa watu, wakiwepo waendesha pikipiki ambao waliongoza msafara hadi viwanja vya msikiti mkuu wa Arusha.
Lowassa alifanya kazi hiyo ya harambee ya kuchangia mradi wa ujenzi wa jengo la ghorofa tano la msikiti huo litakalokuwa na shule ya sekondari, msikiti na kituo cha watoto yatima.
Barabara ya Uhuru, ambayo msafara huo ulipita ukiongozwa na pikipiki za polisi, ilifungwa na wafuasi wa Lowassa, ambao magari yao yalikuwa na nembo za ‘Team Lowassa’ na ‘Lowassa FU’ huku, wengine wakiwa na magari binafsi na waendesha pikipiki.
Lowassa alitua uwanja mdogo wa Arusha saa 7:30 mchana na alifika viwanja vya msikiti mkuu, saa 8:35 mchana na kulifanyika harambee ya kuchangia kituo cha elimu cha kiislam na msikiti wa Patandi na kupokelewa na umati huku wakiimba “rais, rais, rais” na kupokelewa na sheikh wa mkoa wa Arusha, Sheikh Shaaban Juma.
Katika msafara huo, Lowassa aliambatana na kaimu mkuu wa mkoa, Christopha Kangoye, mkuu wa wilaya ya Arumeru, Hasna Mwilima, mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba na mbunge wa viti maalum (CCM) mkoa wa Arusha, Namelock Sokoine.
Pia walikuwepo baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) wa wilaya, wafanyabiashara wakubwa wa mkoa wa Arusha, Mwanza na Kilimanjaro, sambamba na watu kadhaa wanaotarajiwa kugombea ubunge katika majimbo ya Arusha mjini, Arumeru Mashariki, Arumeru Magharibi, Monduli, Londigo na Ngorongoro.
Amshukuru Dk Bilal
Akizungumza katika harambee hiyo, Lowassa alisema si jambo dogo kupewa fursa kumwakilisha makamu wa Rais Dk Bilal katika hafla hiyo.
“Baada ya Makamu wa Rais kuniomba kuja kumwakilisha hapa,  nilisita kidogo kwanza kutokana na kuwa  hapa ni nyumbani, pia bado nipo kifungoni na pia nimekuwa nikialikwa katika harambee kadhaa za misikiti mkoani hapa na kushindwa kufika,” alisema ambaye amefungiwa kujihusiaha na shughuli za uchaguzi pamoja na makada wengine watano.
Alisema hata hivyo, baadaye alikubali kwa kutambua jambo ambalo anamwakilisha Makamu wa Rais ni la maendeleo kwa wananchi wa mkoa mzima wa Arusha na Taifa.
Avunja ukimya
Lowassa akizungumza na mamia ya watu waliohudhuria katika hafla hiyo, alisema amekuja Arusha akiwa na taarifa njema kuwa, Mei 24 atazungumza neno kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Aliwataka wakazi wa Arusha kumuunga mkono, siku hiyo kwa kujitokeza kwa wingi  kumsikiliza.
“Mei 24 nitatoa neno siku hiyo na mtu akikuuliza unakwenda wapi mjibu nakwenda kwenye safari ya matumaini,” alisema Lowassa huku akishangiliwa na umati wa watu.
Lowassa alipongeza wakazi wa Arusha kwa umoja wao, wanaoendelea kuuonyesha bila kujali itikadi zao, dini wala rangi, kutokana na kuhudhuria kwa wingi katika harambee hiyo.
“Hii ndio Arusha ninayoijua mimi, tumeishi kwa upendo na amani miaka mingi, tusikubali kugawanywa kwani sote ni binadamu tulio sawa,” alisema
 Achangisha 235 milioni
Katika harambee hiyo, zaidi ya Sh235 milioni zilichangwa, wakati Lowassa, Makamu wa Rais na marafiki zake, walichanga Sh105 milioni.
Lowassa alikabidhi Sh50 milioni taslimu kwa sheikh wa mkoa wa Arusha, ikiwa ni mchango wake, makamu wa Rais na marafiki zake huku na kuahidi Sh50500 milioni.
Katika  harambee, hiyo Sheikh wa mkoa, alijisahau na kumuita Lowassa ‘Mh Rais’, na kusababisha umati wa watu kushangilia. Fedha nyingine Sh130 milioni zilichangwa.
Baadhi ya wachangiaji walikuwa ni marafiki wa Lowassa walioongozwa na Mathias Manga, ambaye ni mjumbe wa NEC wa wilaya ya Arumeru, ambao walitoa Sh20milioni, Hussein Gonga Sh7 milioni na Mkandarasi Jeremiah Ayo alitoa Sh5milioni.
Mgombea watarajiwa wa ubunge, Mustapha Panju alitoa Sh6 milioni, Sioyi Sumari (Sh7 milioni), Kim Fute (Sh3 milioni), Philemon Mollel (Sh5 milioni), mbunge Peter Serukamba (Sh3 milioni) na mjumbe wa NEC kutoka jimbo la Busega, Dk Raphael Chegeni alichanga Sh1 milioni sawa na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Namelock Sokoine.
Gharama
Awali akizungumza kabla ya kuanza kwa harambee hiyo, katibu wa Bakwata mkoani Arusha, Juma Masoud alisema kuwa mradi wa ujenzi wa msikiti huo unatarajiwa kugharimu Sh1 bilioni hadi kukamilika.
Alisema kuwa mradi huo ni miongoni mwa miradi mikubwa ambayo wanatarajia kuitekeleza na kwamba ujenzi utahusisha ghorofa tano na ndani yake kutakuwa na kituo cha watoto yatima.
“Waumini katika msikiti huu kwa sasa wanakbiliwa na changamoto ya sehemu ya kufanyia ibada hivyo kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuokoa tatizo hilo,” alisema.
Alisisitzia kuwa awamu ya kwanza ya mradi huo unataraji kugharimu jumla ya kiasi cha Sh200 milioni na alimpongeza Lowassa kwa kujitoa katika juhudi za kusaidia maendeleo ndani ya jamii.
Naye Sheikh Shaaban alisema harambee hiyo inahusu wakazi wote wa Arusha kwani sekondari itakayojengwa haitakuwa ya dini moja hivyo, aliwashukuru wote waliochangia na mungu atawalipa.
Mwananchi

9 comments:

Anonymous said...

Dr. Bilal hizi ni kampeni tupu. Sasa. Mzee Lowassa tunaloomba, sisi WaTanzania unaotuomba kuja uwanjani hiyo May 24 ambayo ni karibu tu. Ni vyema ukaanza na mazungumzo ya kueleweka ni 1. kipi kilikusibu ukakubali kuachia nafasi kubwa ya uwaziri Mkuu!! Barua uliyomwandikia mkuu wako tunayo na alibidi akukubalie kuepusha gumzo. 2. Jambo jilo la RICHMOND hewa liliigharimu Tanzania kiasi gani katika nyanja ya umeme. 3. Hapa majuzi ESCROW wameziibua za kutosha na zinahusiana na swala la Umeme pia. Kweli Tanzania imekuwa jalala ni haki kweli tukose umeme mathubuti. Wote waliohusishwa na ESCROW ni walewale ndani ya serikali unayotaka kuiongoza wakati na wewe ulikuwa na matatizo! Hivi kweli sisi wananchi tunaoshabikia tunatarajia nini? Tanzania inahitaji kiongozi atakayesema BASI IMETOSHA. Waache mara moja na kama hukumu itoke.TUMECHOSHWA na mikataba isozaa matunda.

Anonymous said...

Mdau hapo juu una uhakika na ulichokisema? Wewe ni daktari wake au!?

Anonymous said...

I don't have to be his doctor to be sure of what I say bit I will be more than happy to debate you on this. Bring it on...

Anonymous said...

Lowssa has a lot to explain to the Tanzanian people. We can't award incompetent an unethical people for destroying our country.

Anonymous said...

Kuna tofauti kubwa kati ya mnyama na binadamu, mnyama hana utu na pia inawezekana nafsi kama tulivyo sisi wanadamu, Binadamu tunajielewa na tunao uwezo wa kujua yapi mabaya na yasiyo mabaya. Natatizwa na mdau wa kwanza hapo juu anayeongelea afya ya Lowassa, nafikiri maoni yake ni abusive na very offensive si kwa Lowassa ila hata kwa mtu yeyote atakayesoma ataona hayo maoni ni disgusting. Kwa utamaduni wowote ule kwanza huwezi kukisia tu Fulani ana tatizo gani la kiafya kwa sababu kwanza wewe siyo daktari hata kama ni daktari ugonjwa wa mtu ni siri yake, pili kama wewe si daktari utajuaje ugonjwa wa mtu unless kama amekwambia. Sasa mdau wa kwanza hapo juu unaposema Ikulu si ya wagonjwa unaonyesha jinsi gani akili yake ilivyofika ukomo wa kufikiri. Ugonjwa unakuja kwa njia nyingi na imani kabisa hata wewe ukienda mara kwa mara kwa check up si rahisi ukakosa hata defect au kaugonjwa kadogo hata kama leo hutakuwa nao kesho inawezekana ukapata ugonjwa (kumbuka binadamu siyo vyuma). Una maana ukisema ikulu si pa wagonjwa ina maana unam-disqualify hata rais wetu aliyepo hapo kwa sababu alishawahi kuanguka jukwani na alishawahi kulazwa hospitali???? Je unajua ugonjwa anaoumwa Lowassa, maana inawezekana wewe ni daktari? Kwanini unajenga chuki na mtu anayefikiria kugombea uongozi, kwani kugombea uchaguzi si haki ya kila mtanzania mwenye umri unaofaa kugombea na mwenye akili timamu??? Hata wewe unaweza kugombea maana hiyo ndiyo demokrasia na sisi watanzania tutachagua mchele au chuya, maana tuna uwezo wa kufikiri hivyo kama ukiuza sera zako na tukiku-screen tutajua kama unafaa au la. Simtetei Lowassa ila kama DJ Luke blog yake inavyotaka kuwa tusiharibu siku kwa matusi au kashfa au maneno yasiyo na uhakika ni haki yangu kuandika jinsi gani sipendezwi( Na imani watanzania wengi pia hawapendezwi na maoni yako) na lugha chafu, isiyo ya kistaarabu na yenye kuudhi.

Anonymous said...

Wa Tanzania umefika wakati muafaka wa kutambua matatizo tuliyo nayo ni ukiritimba wa uongozi tulio nao waliobobea na hawataki kuachia ngazi! Tuna vijana wengi sana wanaweza kutukomboa. Ikulu kuna nini jamani? Hivi zipo mashine a kufyatua hela nini?? Chama tawala tunaomba mkubali kupumzika.. Imetosha..

Anonymous said...

Waziri Mkuu aliyejiuzulu shauri ya kuhusika na kashfa mbaya ya rushwa ambayo inahatarisha usalama wa nchi. Kustaafu na kujiuzulu ni mambo mawili tofauti

Anonymous said...

Anon of May 16, 2015 at 9:44 PM (Team Lowassa),

Your candidate has nothing new to offer. He's a leader of the past and one of the least qualifying presidential candidate ever seen in my life. He has been in the system for over thirty years but what we see from his records is ufisadi. Not only that, he's sick and he knows that his health will not allow him to run day to day presidential responsibilities.

I will tell you what Team Lowassa, let us play a game. It's called "Who's smarter than a Lowassa supporter. Let me know when you are ready or stay silent because you are full of bullshit.

Anonymous said...

Hivi yule kiongozi mahiri aliyewaibia Watanzania mamilioni ya $ Kwa manufaa yake binafsi hadi leo Watanzania wapo gizani ni binaadamu au mnyama. Hivi unadhani Watanzania hawana haki ya kumuuliza au kupata maelezo toka kwake? You sounds like you are so blinded by ignorance that you can't see things straight.