Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi jimbo la Uzini (CCM), Mohamed Raza ( kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya mustakabali wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Vincent Tiganya.
KADA wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Mohammed Raza, ameshtushwa na baadhi ya wagombea wa nafasi
ya urais wa Jamhuri ya Muungano kumwaga mabilioni yafedha chafu Zanzibar ili kuwashawishi baadhi Wajumbe wa chama hicho
kuwaunga mkuno katika mbio hizo.
Raza ambaye ni
Mwakilishi wa Uzini, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, wakati
alipozungumza na wandishi wa habari, kuhsu mustakakabali wa kupatikana Rais wa
Jamhuri ya Muungano kwa vile hilo ni suala nyeti katika kipindi hiki cha
kuelekea uchaguzi mkuu.
“Suala hili
lina unyeti wake kwani linagusa hadi majeshi na mahakama amabao nao wanapaswa
kujua sifa za rais ajaye, hivyo haitakuwa busara kwa rais wa nchi apatikane kwa
njia ya rushwa.
Alisema hivyo
kwa vile kuna baadhi ya wawagombea wanafasi hiyo, wakishirikiana na
wafanyabiashara tayari wanaendelea na mchezo huo mchafu wa kutoa rushwa
waziwazi huku hata Kamati Kuu ya Chama Ikishindwa kukemea vitendo hivyo vya
hatari kwa nchi.
“Nazungumzia
chama changu, tumeingia kwenye uchaguzi mkuu, naamini bado tunakazi ya
kutekeleza Ilani ya chama cha mapinduzi hatujamaliza kazi, sasa kama sisi viongozi tunaona
mabilioni ya rushwa yakiingizwa dhahiri bila ya kukemewa imenishtua,”alisema.
Raza, alisema
kitendo cha kupatikana rasi iliyetokana na misingi ya rushwa, itafika wakati
rais huyo atashindwa kuwa na maamuzi ya kuongoza nchi na baadala yake atakuwa
akitekeleza matakwa ya magenge ya watoa rushwa.
“Tunapompata
rais ambaye amechaguliwa kwa misingi ya rushwa Watanzania wajue kuwa atakuwa
akielezwa na waliomuingiza madarakani kwamba mchague huyu au yele ashike wizara
fulani kwa ajili ya maslahi yao ,
lakini pia chama changu lazima kijue kuwa kuna Ukawa na CUF ambao nao wanataka
kuingia madarakani,”alisema Raza.
Akizungumzia
Suala Akaunti ya Tegeta Escrow, Raza, alisema kuwa Wazanzibar wanamtaka Waziri
wa Fedha, atoe tamko atalifidiaje pengo Zanzibar kukosa misaada
kutokuna naTanzania kuwekewa vikwazao na wahisani kutokana na kashfa ya Akaunt
ya Tegeta Escrown.
Alisema, hivyo
kwa vile kashfa hiyo haiwahusu Wazanzibari, kwani halikuwa suala la
muungano bali lilikuwa la Bara.
Hata hivyo,
Raza, alisema bado viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibarr, wanatakiwa
kuacha woga na baadala yake wajenge hoja kwa kuwaambia wahisani kuwa suala hilo haliwahusu
Wazanzibari.
“Mwaka
1995 Zanzibar ,
iliwekewa vikwazo na huku bara ikidai kuwa iliambiwa na wahisani isiwape
misaada, lakini kwa hili la Escro, viongozi wa Zanzibar walitakiwa
kujenga hoja kwamba haliwahusu, angalia pale hakukua hata na Mzanzibari
aliyehusika katika kashfa ya Tegeta Escro,”alisema Raza.
Raza,
alisisitiza kuwa hata wakati wa EPA wazanzibari hawakuhusika lakini waliingizwa
akibainisha kuwa hayo yote yanatokea kutokana na woga wa viongozi wa Serikali
ya Zanzibar .
Aidha, Raza
amesistiza kuwa alifuatilia suala hilo la vikwazo ili ikiwezekana Zanzibar iweze
kuondolewa vikwazo hivyo ambavyo anaamini haviihusu Zanzibara.
No comments:
Post a Comment