ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 17, 2015

SAFARI ZA RAIS KIKWETE ZAOKOA ZAIDI YA DOLA LAKI MOJA ZA KIMAREKANI


 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dokta Othman Kiloloma (kushoto) akizungumza na wandishi wa Habari (pichani hawapo)  baada ya hitimisho la  Mkutano wa nne wa mafunzo ya Upasuaji wa Ubongo , uti wa mgongo na mishipa ya fahamu, Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid, uliomalizika hivi karibuni. ambapo wakishirikiana na Wataalamu  madaktari bingwa wa Chuo cha Weill Cornell toka Marekani kufanya upasuaji wa mgongo kwa kutumia mashine ya kisasa, ambapo Watanzania  21 wamefanyiwa  upasuaji wa magonjwa hayo wakishirikiana na madaktari toka Tanzania , Uganda, Rwanda, Southi Afrika, Marekani na Ulaya. Dokta Othman Kiloloma, alimshukuru Rais Jakaya Kikwete ambaye aliye waweka karibu na wenzao wa Chuo cha Marekani na kuwashukuru wenzao wa chuo cha marekani kwa kuwawezesha kufanyika upasuaji huo. (wakwanza kulia) ni Mkuu wa Idara ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu Dk.Hamisi Shabani,ambaye aliwaeleza waandishi hao kua mgonjwa mmoja kufanyiwa upasuaji anagharimu kiasi cha dola elfu moja za upasuaji huo nahaihusiani na mambo mengine.na katikati ni Profesa Philip Steg toka Chuo cha Marekani nayeye alipata nafasi ya kuongea na waandishi hao na kuwashukuru Wataalamu wa Moi (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dokta Othman Kiloloma (wapili) kushoto na kuanzia kulia ni Mkuu wa Idara ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu Dk.Hamisi Shabani anaye fatia ni Profesa Philip Steg toka  Chuo cha Weill Cornell  Marekani na kushoto ni Menneja ea Taasisi ta Moi Almas Jumaa.
 Madaktari wakiwakatika Upasuaji na ikiongozwa Dk, Japhet Ngerageza
 Mashine ya kisasa yenye thamani shilingi mil. 700 iliyotolewa msaada na Weill Cornell toka Marekani ikikumika kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania kwa Muungano wa jitihada za Rais Jakaya Kikwete
 Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) wakishirikiana na madaktari bingwa wa Chuo cha Weill Cornell toka Marekani kufanya upasuaji wa mgongo kwa kutumia mashine ya kisasa ambapo wagonjwa 21 wamefanyiwa  upasuaji wa magonjwa hayo.  Dar es Salaam
 Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) wakishirikiana na madaktari bingwa wa Chuo cha Weill Cornell toka Marekani wakionyeshana jambo wakati walipokuwa wafanya  upasuaji wa mgongo kwa kutumia mashine ya kisasa ambapo wagonjwa 21 wamefanyiwa  upasuaji wa magonjwa hayo.  Dar es Salaam
Madaktari wakiwa katika chumba cha Upasuaji

No comments: