ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 23, 2015

SAMAEL ACADEMY PEMBA YAPATA MSAADA

MKUU wa Chuo cha ZCBE Zanzibar, Abdull-wahabi Said Bakar akielezea namna ya kuongeza ushirikiano baina ya chuo chake na taasisi ya Samael Academy, kwenye mkutano maalumu wa kuangalia kazi zinazofanya na taasisi hiyo.
AFISA mdhamini wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Pemba Ali Nassor Mohamed, akizungumza kwenye mkutano maalumu wa kuangalia shughuli zinazofanywa na taasisi ya Samael Academy, kulia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo sheikh Nassor Said Al-rawahy na kusoto ni mkuu wa chuo cha ZCBE Abdull-wahabi Said Bakar.

AFISA mdhamini wizara ya Habari Pemba Ali Nassor Pemba, akiangalia foronya ya kisasa iliotengeneza na wanafunzi waliochini ya taasisi ya Samael Academy, wakati afisa huyo akikagua kazi za amali zinazofanya na wanafunzi waliopo kwenye taassi hiyo, kushoto ni Mkuu wa chuo cha ZCBE Abdul-wahabi Said Bakar na kulia ni wanafunzi wa ushoni wa Samael.
MDHAMINI wa taasisi ya Samael Academy sheikh Said Abdall Nassor, akimuonyesha vyarahani Afisa Mdhamini wizara ya habari Pemba Ali Nassor Mohamed kulia, ambapo msaada huo umetolewa kwa kikundi cha ushoni cha ‘Taratibu tailoring’ na Mwenyekiti wa samael sheik Nassor Said Rawahy.
MWALIMU Salim ambae ni mkufunzi wa ufundi wa seremala akimuelezea jambo Afisa Mdhamini wizara ya habari utamaduni utalii na Michezo Ali Nassor Mohamed, wakati alipowatembelea kuangali kazi zinazofanywa na vijana waliopo kwenye taasisi ya Samael Academy, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments: