Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Laurent Kavakure jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro.
Ujumbe wa Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakifuatilia mazungumzo hayo kabla ya kupata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Waziri Membe kwa heshima ya mgeni wake.
Ujumbe wa Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakifuatilia mazungumzo hayo kabla ya kupata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Waziri Membe kwa heshima ya mgeni wake.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA
MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Nukushi: 255-22-2116600 |
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb.), leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Burundi, Mhe. Laurent Kavakure jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency,
Kilimanjaro. Mhe. Kavakure aliwasili nchini tarehe 03 Mei
2015.
Wakati huo huo, Mhe. Membe ataongoza ujumbe wa Mawaziri wa Mambo ya Nje
wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenda Burundi siku ya Jumatano tarehe
06 Mei 2015 kufanya mazungumzo na Serikali ya Burundi kuhusu hali ya kisiasa
inayoendelea nchini humo.
-Mwisho-
Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
04 Mei 2015
No comments:
Post a Comment