ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 23, 2015

TUME YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YATEMBELEWA NA MWANADIASPORA KUTOKA NCHINI MAREKANI

Mwanadiaspora Walter akiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi mkuu wa Tume ya Sayansi na Tekinolojia - COSTECH (http://www.costech.or.tz) Dr. Hassan Mshinda. Mazungumzo ambayo yalilenga shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo kwenye mambo ya tekinolojia na jinsi gani wana-diaspora wanavyoweza kuchangia katika kuleta maaendeleo ya tekinolojia nchini kwao.  Mwanadiaspora aliwaambia kwa jibu la haraka anachoweza kufanya kuwatafutia vitabu kutoka kwenye vyazo vyake mbali mbali kama universities, library na maduka ya vitabu na kuwatumia katika kuitikia mwito kusaidia nyumbani.
Mdau Walter na Jacqueline mkuu wa mahabara ya ubunifu akijaribu kuangalia mojawapo ya kifaa kilichotengenezwa na vijana wakitanzania katika ubunifu wao wa mambo ya 3D printing.
Picha ya pamoja na wachapakazi wa BUNI Hub (http://www.buni.or.tz) ambayo ni sehemu kubwa ya ubunifu wa vifaa, ujasiriamali na maendeleo katika jamii. BUNI hub ni sehemu ya kisasa ambayo inamuongozo wa vijana wenye mawazo endelevu katika jamii.
Mdau walter akitembezwa katika mitambo inayoendeshwa na kitengo cha TERNET (http://www.ternet.or.tz). TERNET ni mtandao wa taasisi zote za utafiti nchini kwa kutumia mtandao wa interneti. Ternet hutumia mkonga wa taifa (fiber Optic) katika kuziunganisha taasisi hizi za kiserikali. 

Ikiwa ni picha ya pamoja na watendaji kazi wa kitengo cha Ternet. Mdau Walter alifurahishwa na uchapaji wao katika kuunganisha vyuo na tasisi hizo serikali kwa zinarahisisha ufanisi wa kazi pamoja na suala zima la utafiti.