Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya
Jinai (ICC), imeitaka Afrika Kusini kumkamata rais wa Sudan Omar
Al-Bashir ambaye anaripotiwa kusafiri kwenda nchini humo kuhudhuria
mkutano wa Muungano wa nchi za Afrika ambao unaanza leo Jumapili.
Kwenye taarifa yake, ICC imesema
kuna waranti mbili za kumkamata Bashir anayetakiwa na mahakama hiyo
kuhusiana na tuhuma za kuhusika na uhalifu ulitokea katika jimbo la
Darfur na kwamba anakabiliwa na kesi inayohusiana na uhalifu wa
kivita na mauaji ya halaiki.
Kama mwanachama wa ICC, Afrika
Kusini inastahili kumkamata Bashir ikiwa atasafiri kwenda nchini
humo, agizo ambalo limetoka huku Umoja wa Afrika ukiwa umeweka wazi
kuwa haupo tayari kushirikiana na mahakama hiyo kwa madai kuwa mara
zote imekuwa ikiwaonea viongozi wa Afrika. Hata hivyo Bashiri
amepokelewa nchini Afrika Kusini.
1 comment:
Go to hel Icc
Post a Comment