ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 17, 2015

BANZA STONE YUKO HOI, HAZUNGUMZI, AMEGOMA KULA CHAKULA NA KUNYWA DAWA, WASANII WENGI WAMEMTENGA – MAMA MZAZI

Mama mzazi wa muimbaji wa muziki wa dance, Banza Stone amesema mwanae afya yake imezidi kuzorota na sasa amegoma kula chakula wala kunywa dawa.

Akiongea na Ripoti ya kipindi cha Ubaoni cha EFM juzi, mama huyo alisema hadi siku hiyo Banza alikuwa amegoma kula kwa siku tatu mfululizo.
Aliongea kuwa pamoja na kuugua hivyo bado wasanii wenzake wameshindwa kwenda kumjulia hali.
“Mpaka sasa sijamuona mtu yeyote aliyekuja kumshughulikia na kumwangalia, wamemwacha hivi hivi. Na mimi siwezi kuwalaumu kwanini hamjaja kumwangalia, kila mtu na moyo wake, mwenye kuja atakuja, mimi ntahangaika na mtoto wangu mpaka pale atakapoamua mwenyezi Mungu,” alisema Mama Banza.
Kwa mujibu wa kaka yake, Banza, Jabir Masanja, anasumbuliwa na fangasi kichwani mwake na dawa anazotumia ni kali kiasi cha kumpotezea hamu ya kula.
Jabir amewaomba wadau wa muziki na mashabiki wake walioguswa kumchangia chochote Banza kwa kutuma chochote kutumia namba: 0715407088 au 0753786016.

4 comments:

Anonymous said...

Wewe mama na mwanao nyote wendawazimu. Umeshindwa kumpa maadili mema mwanao mpaka amekuwa teja. Banza hajatumwa na msanii yeyeto kutumia madawa ya kulevya na wkati anaanza kuyatumia hakutoa taarifa kwa wasanii wenzake. Iweje leo wasanii walaumiwe kwa kumtenga? Kama alipata pesa ya kununua madawa, kwa nini akose pesa ya matibabu?

Anonymous said...

Duh,kali hiyo

Anonymous said...

hivi Tanzania family member akiumwa ni jukumu la kila mtu kumsaidia eeh!

Anonymous said...

Kweli wewe wakwanza na wapili mnavisa vyenu. Mbona nyie juzijuzi mlimchangia mtoto wa mama nanii akatibiwe India.