Chama cha Wananchi (CUF) kimetangaza majina ya wagombea ubunge na uwakilishi walioteuliwa na Baraza Kuu la chama hicho.
Baraza hilo lilikutana juzi jijini Dar es Salaam na kuchambua majina ya wagombea waliopitishwa kwenye kura za maoni katika majimbo mbalimbali nchini.
Wakati majina hayo yakitangazwa, baadhi ya wafuasi wa chama hicho wamelalamikia uteuzi huo kuwa haukuwa huru na haki.
Aidha, katika Jimbo la Mkanyageni, Pemba, wanachama wa chama hicho kwenye kura ya maoni ‘walimtema’ Mbunge wao wa sasa, Mohamed Habibu Mnyaa, lakini Baraza Kuu limemrejesha kugombea nafasi hiyo.
Wagombea walioteuliwa kuwania nafasi za uwakilishi na majimbo yao kwenye mabano ni Ismail Jussa Ladhu (Mji Mkongwe), Ali Haji Mwadini (Jang’ombe), Moh’d Khalfan Sultani (Kikwajuni), Maulid Suleiman Juma (Chumbuni), Amina Rashid Salum (Kwamtipura),Yussuf Idrisa Mudu (Magomeni), Ali Hamad Ali (Mpendae).
Wengine ni Khamis Rashid Abeid (Amani), Hassan Juma Hassan (Kwahani), Abdilahi Jihad Hassan (Magogoni, Juma Duni Haji (Bububu), Saleh Khamis Omar (Mfenesini), Nassor Ahmed Mazrui (Mtoni), Nassor Ahmed Mazrui (Mtoni).
Wengine ni Yussuf Omar Muhine (Dole), Moh’d Hashim Ismail (Dimani), Mansour Yussuf Himid (Kiembe Samaki), Ussi Juma Hassan (Mwanakwerekwe), Sleiman Simai Pandu (Fuoni), Hassan Jani Masoud (Nungwi), Nahoda Khamis Haji (Matemwe), Haji Kesi Haji (Mkwajuni).
Pia wapo Khamis Masoud Nasor (ubunge Jimbo la Chaani), Khamis Amour Vuai (uwakilishi), Khatib Ali Juma (ubunge Jimbo la Tumbatu), Makame Haji Makame (uwakilishi), Rashid Khamis Rashid (ubunge Jimbo la Donge), Seleiman Ahmed Sleiman (uwakilishi), Kombo Mohamed Kombo (ubunge Jimbo la Bumbwini), Zahran Juma Mshamba (uwakilishi), Mohamed Amour Mohamed (ubunge Jimbo la Kitope) na Hassan Khatib Kheir (uwakilishi).
Wengine ni Mwinshaha Shehe Abdallah (ubunge Jimbo la Uzini), Asha Simai Issa (uwakilishi), Adam Ali Wazir (ubunge Jimbo la Koani), Khamis Malik Khamis (uwakilishi), Shaaban Iddi Ame (ubunge Jimbo la Chwaka), Arafa Shauri Mjaka (uwakilishi), Ali Khamis Ame (ubunge Jimbo la Makunduchi) na Jimbo la Muyuni (hajapatikana).
Wengine ni Asha Abdu Haji (uwakilishi), Baswira Hassan Suleiman (ubunge Jimbo la Tumbe), Mmanga Mohamed Hemed (uwakilishi), Rashid Ali Abdalla (ubunge Jimbo la Micheweni), Subeit Khamis Faki (uwakilishi), Haji Khatib Kai (ubunge Jimbo la Konde), Issa Said Juma (uwakilishi), Khatib Said Haji (ubunge Jimbo la Mgogoni), Abubakar Khamis Bakar (uwakilishi) na Juma Kombo Hamad (ubunge Jimbo la Wete).
Wengine ni Dk. Suleiman Ali Yussuf (uwakilishi), Mbarouk Salum Ali (ubunge Jimbo la Ole), Hamad Masoud Hamad (uwakilishi), Rajab Mbarouk Mohamed (ubunge Jimbo la Gando), Said Ali Mbarouk (uwakilishi), Othman Omar Haji (ubunge Jimbo la Mtambwe), Khalifa Mohamed Issa (ubunge Jimbo la Kojani), Hassan Hamad Omar (uwakilishi), Hamad Salum Maalim (ubunge Jimbo la Chakechake) na Omar Ali Shehe (uwakilishi).
Wengine ni Yussuf Kaiza Makame (ubunge Jimbo la Chonga), Khamis Faki Marango (uwakilishi), Mohamed Juma Khatib (ubunge Jimbo la Ziwani), Mohamed Ali Salum (uwakilishi), Ahmed Juma Ngwali (ubunge Jimbo la Wawi), Khalifa Abdalla Ali (uwakilishi), Juma Hamad Omar (ubunge Jimbo la Chambani), Mohamed Mbwana Hamad (uwakilishi), Yussuf Salim Husein (ubunge Jimbo la Kiwani), Hija Hassan Hija (uwakilishi) na Abdallah Haji Ali (ubunge Jimbo la Mkanyageni) na Tahir Aweis Mohamed (uwakilishi).
Wengine ni Mohamed Habibu Juma Mnyaa (ubunge Jimbo la Mkoani), Seif Khamis Mohamed (uwakilishi), Ali Khamis Seif (ubunge Jimbo la Mtambile, Abdallah Bakar Hassan (uwakilishi) na Masoud Abdalla Salim.
Jimbo la Mtambile, Pemba ni miongoni mwa baadhi ya majimbo ambayo wafuasi wanakilalamikia chama chao kwa kumteua mtu ambaye siyo chaguo lao.
“Tunawasiwasi mkubwa kuwa katika baraza kuu imetumika rushwa na upendeleo kwani mgombea ambaye tumempigia kura nyingi siyo tuliyeletewa,” alisema Suleiman Salim mkazi wa jimbo hilo.
Alisema baada ya wananchi wa jimbo hilo kupata taarifa kuwa baraza kuu la chama limemteuwa Masoud Abdallah kuwa mgombea wa jimbo hilo wakati wananchi wa jimbo hilo awali walipiga kura ya maoni na kumchagua kwa kura nyingi Ali Bakari Khamis ambaye jina lake halikurudi mtafaruku mkubwa umezuka jimboni humo.
Alisema wanachama zaidi ya 300 jana walijikusanya na kuweka kadi zao za CUF katika kiroba kwa lengo la kutaka kurejesha kadi hizo na kutoka katika chama hicho kutokana na upendeleo uliotumika kuwapata wagombea.
Alisema walifanikiwa kuwatuliza wafuasi hao na kuwataka kutumia hekima na busara kufikisha malalamiko yao katika sehemu husika.
“Kama CUF kikishindwa kutuletea mgombea ambaye tulimtaka na kumpigia kura ya maoni hatutorizika kabisa na uamuzi uliofanywa na baraza kuu na tunasema tutaamua katika uchaguzi mkuu wakati wa kupiga kura” alisema Salim ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu Jimbo la Mtambile.
Akizungumzia uteuzi wa wagombea hao mbele ya waandishi wa habari visiwani hapa jana, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho, Omar Ali Shehe, alisema utaratibu uliotumika kuwatafuta wagombea haukizingatia kura za maoni pekee bali pia ulizingatia vigezo nyengine.
“Kigezo kikubwa katika uteuzi huu wa wagombea ni kura za maoni ambapo wananchi majimboni waliwapigia kura wagombea na kupatikana watu watatu bora ambao walipelekwa baraza kuu ndilo lenye maamuzi ya mwisho lakini pia baraza kuu liliangalia uwezo na sifa za wagombea” alisema Omar.
Omar ambae pia ni mwakilishi wa jimbo la Chakechake Pemba, alifahamisha kuwa baadhi ya wagombea ambao majina yao yalipita katika uchaguzi wa kura za maoni majimboni lakini majina yao hayakupita kutokana na sababu mbalimbali ambazo hakuzitaja.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment