Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibroad Slaa akiwa na Mshauri wa Masuala ya Uchumi, Sayansi na Maendeleo ya Jamii katika ulimwengu wa dijiti (digital), Dk. Mario Voigt, walipokutana Villa La Collina, Milan kwa ajili ya kujadiliana na kubadilishana uzoefu kuhusu namna bora ya kusimamia uchumi unaonufaisha wananchi hususan kwenye nchi zenye utajiri wa rasilimali lakini watu wake wanakabiliwa na umaskini, kama Tanzania. Dk. Voigt ni mtaalam katika eneo hilo, akitokea iliyokuwa Ujerumani Mashariki, ambayo uchumi wake ulikuwa ukiendeshwa na sera za kisoshalisti kabla ya kupitia mabadiliko makubwa kutoka hali duni na sasa sehemu hiyo ni mojawapo ya jamii zenye maendeleo makubwa ndani ya Ujerumani. Dk. Slaa yuko ziara ya kikazi barani Ulaya kwa siku 7. (Na mpiga picha maalum).
2 comments:
hivi jamani hawa viongozi washauri wao wako wapi? sasa suite gani huyo mzee slaa amevaa, tai na shati kachanganya rangi. halafu koti kubwa limemvaa. haya mambo ya aibu. washauri wake inabidi vitu kama hivyo waviangalie jamani. mzee slaa ni public figure anatakiwa apendeze. ushauri wa bure na kuelimisha tu
Wenzako wanakampeni wewe bado unazurura ulaya
Post a Comment