ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 12, 2015

MAKOSA YA WANAWAKE, WANAUME KATIKA KURIDHISHANA


WAZEE wenzangu mwajionaje na hali? Hii ni safu iliyoboreshwa ya Sindano ya Mahaba! Kazi yake kubwa ni kuelimisha jamii, hasa ya watu wanaozidi miaka kumi na nane, katika masuala ya mapenzi na uhusiano.

Kwa mara nyingine kona hii imekuja kutatua matatizo ya wengi katika uhusiano. Nitakuwa nikiongea na wasomaji akina baba, akina mama na wale wasiofikia hapo kupitia safu hii.Kwa kuanza tu, najipa ujasiri wa kusema kuwa, ndoa nyingi siku hizi zimekuwa zikiyumba kwa sababu tu ya lawama za wanandoa kutoridhishana wawapo kwenye safari yao ya tendo la ndoa. Hii inaniuma sana mimi!

Ikumbukwe kuwa, mashua pia inahitaji upepo kwenye safari yake haitegemei mashine tu kama wengi walivyozoea. Msemo huu una maana kwamba, mwanamke au mwanaume usikae kusubiri stimu itakuja wakati wa tendo, jishughulishe na mwenzako naye ajishughulishe na wewe.Hapa unatakiwa kumpa ushirikiano mwenzako pale anapokuwa anakuhitaji lakini wewe haujisikii hata kidogo.

JIFUNZE HAYA
Wewe mwanamke, inawezekana mumeo ana maradhi yanayosababisha kushindwa kukufikisha kwenye mwisho wa safari yako lakini zipo njia mbalimbali ambazo mke naye anatakiwa kumuelewa mumewe na kumpa nafasi ya kumsaidia.

FANYENI HIVI
Kama ni mwanamke unamuona mumeo hana kiu na safari kaa naye, zungumza naye tena kwa upole kabisa ili ujue tatizo lake. Baada ya hapo muelekeze amfanyie nini ili kiu yake irudi na umpe ushirikiano wa hali na mali.
Mume naye, jipe nafasi kwa mkeo, jaribu kutumia yale uliyojaliwa na Mungu ili kumridhisha na kuifanya safari yenu kuwa nzuri na ya amani.

EPUKA LAWAMA
Wanandoa, ukishamuona mwenzako hana hamu ya chakula chako, acha lawama na shutuma kama vile kumwambia; ulikuwa kwa hawara zako huko’ au; ‘umetoka nje ya ndoa wewe’. Hilo ni kosa kubwa sana mnapokuwa faragha kwani hata kama angeweza kushawishika na kushiriki, kila kitu kinasinyaa na kuwa kama mgonjwa.

MWANAMKE RUDISHA MAFUNZO ULIYOPEWA NA KUNGWI WAKO
Hapa nakukumbusha wewe mwanamke kuyarudia yale mafundisho uliyopewa na kungwi wako kwani mwanamke unapoona mumeo hakukati kiu ni vyema ukakaa naye na kutafuta tatizo labda anaumwa au ana msongo wa mawazo, mueleze ili atambue analolifanya halikufurahishi, pia mpe nafasi na njia ya kukufurahisha halikadhalika na wewe mpe nafasi ya kumrudisha kwenye hali ya kufurahia safari yenu.

Tatizo wanawake wengi mmekuwa mkitaka kuchezwa kwenye kitchen party tu kwa ajili ya kutuzwa zawadi badala ya kusikia maelekezo ya namna ya kuishi na mume ndani ya nyumba. Mbaya sana!

Wiki hii naishia hapa, kama una tatizo linalokusumbua unahitaji ushauri kutoka kwangu nipigie nami nitakuandikia hapa kila kitu. GPL

No comments: