ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 12, 2015

Mpango Mbaya ya Mwanaafa Kurushwa Mlimani City


KATIKA kutafuta ubora wa filamu kuelekea kimataifa filamu kubwa ya Mpango Mbaya inayowashirikisha wasanii walioibuliwa na mradi wa kuibua vipaji nchini nzima wa Tanzania Movie Talent 2014(TMT) inatarajia kurushwa katika jumba la Sinema Mlimani City tarehe 12.June 2015 anasema Staford Kihore.
“Hatua ya kwanza ilikuwa ni kutafuta vipaji halisi na kuwapatia elimu ya uigizaji, kupitia TMT na hatua ya pili ni kuwachanganya na wasanii waliopo katika tasnia pili ni kwenda kimataifa kwa filamu yao ya Mpango Mbaya kurushwa katika jumba la sinema,”anasema Kihore.

Filamu hiyo inayobebwa na Mwanaafa Mwinzago imeshirikisha wasanii wale kumi bora kama Isalito na wengine waliotoka katika kinyang’anyiro hicho, na itarushwa kwa siku tatu kuanzia Ijuma hadi Jumapili kisha kuuzwa katika Dvd kama wafanyavyo Ulaya.

No comments: