ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 7, 2015

MTANGAZA NIA YA UBUNGE JIMBO LA KAWE KUPITIA CCM, WAKILI ELIAS NAWERA AHIMIZA VIJANA KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KULA

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Wakili Elias Nawera akizungumza na vijana wa Kata ya Kawe.
 Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Wakili Elias Nawera ambaye ametangaza nia ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia CCM akizungumza na wananchi hasa vijana kwenye fainali ya mpira wa miguu kati ya timu ya Halisi FC na Stand United zilizofanyika viwanja vya Tanganyika Peackers Kawe Dar es Salaam jana ambapo aliwaomba ifikapo Julai 4 mwaka huu kujitokeza kwa wingi kujiandika katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Mgombea nafasi ya ubunge Iringa mjini, Ramadhan Yusuph 'Potipoti' ambaye ametangaza nia akizungumza na wananchi wa Kawe katika fainali hizo.

Mgombea nafasi ya ubunge Iringa mjini, Ramadhan Yusuph 'Potipoti' ambaye ametangaza nia akizungumza na wananchi wa Kawe katika fainali hizo.
Watangania ya ubunge, Wakili Elias Nawera na Ramadhan Yusuph 'Potipoti' (kulia), wakiteta jambo katika fainali hizo.
Vijana wa Kawe wakiangalia fainali hiyo.
Mchezo ukiendelea. Stand Unated ilishinda mabao 5-4.
Mchezo ukiendelea.
Mashabiki wa timu ya Stand Unated wakiwazihaki wenzao wa Halisi FC baada ya kuwafunga kwa kubeba jeneza na msalaba wake.
Mashabiki wa timu ya Halisi FC wakishangia kwa kucheza baada ya timu yao kupata bao la pili.
Watoto wakifuatilia mashindano hayo.

Dotto Mwaibale

TIMU ya Stand United, imeibuka bingwa baada ya kuichapa Halisi FC kwa changamoto ya mikwaju 5-4 katika fainali iliyofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, Stand imezawadiwa jezi seti mbili na sh.  400,000 wakati mshindi wa pili alipata jezi seti moja na sh. 100,000.

Akizungumza kabla ya kuanza kwa fainali hiyo, Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Wakili Elias Nawera ambaye ametangaza nia ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia CCM aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam itakuwa ni Julai 4, mwaka huu.

"Ndugu zangu pamoja na mashindano haya ambayo yanatuunganisha na kutupa burudani naomba Julai 4, mwaka huu kujitokeza kwa wingi kujiandikisha bila kujali muda mfupi utakaokuwepo" alisema Nawera.

Akizungumzia kuhusu watu wanaovamia maeneo ya wazi waliyotengwa kwa matumizi mengine alisema watu wa kwanza kuchukua hatua ni wananchi wenyewe mahali alipo.

Katika fainali hizo, pia alihudhuria mgombea nafasi ya ubunge Iringa mjini, Ramadhan Yusuph 'Potipoti' ambaye ametangaza nia.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)





No comments: