Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime - SACP akitoa elimu juu ya hali ya ulinzi na usalama na matishio ya kiuhalifu katika kikao kilichojumuisha wakuu wa vyombo vya dola Mkoa wa Dodoma, viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dodoma pamoja na viongozi wa dini
Balozi Mstaafu Job Lusinde Mwenyekiti wa Baraza la wazee Mkoa wa Dodoma akiongea jambo wakati wa utoaji elimu iliyotolewa kwa viongozi wa mkoa wa Dodoma ili kuhimarisha ushirikiano na kuondoa machafuko ambayo yanaweza kutokea.
Padre Thomas V. Lali Katibu Mkuu jimbo kuu Dodoma akizungumza kuhusu vitabu vya dini vinayozungumzia masuala ya amani hasa katika kuilinda amani.
Shekhe Ahmad Said akizungumza katika mkutano huo
Na: Lakia Ndwellah wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime – SACP amewataka viongozi wa Tarafa ya Dodoma mjini kuwaelimisha wananchi wanaowaongoza na wanaofanya kazi chini yao juu ya matishio na viashilia vya uvunjifu wa sheria na amani ili wote waweze kuwa na uelewa wa pamoja kuvibaini, kuvizuia na kuvitolea taarifa kwa vyombo vya dola waweze kuwakamata wahusika na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.
Ameyasema hayo wakati akitoa elimu juu ya hali ya ulinzi na usalama na matishio ya kiuhalifu katika kikao kilichojumuisha wakuu wa vyombo vya dola Mkoa wa Dodoma, Uongozi wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Katibu Tarafa, Watendaji wa Kata, Watendaji na Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa, Viongozi wa Dini, Mwenyekiti wa Baraza la wazee Dodoma, Mwenyekiti wa TCCIA, Mameneja wa Hoteli mbalimbali, Wakuu wa Idara na Taasisi mbalimbali na Wazee maarufu.
Kamanda MISIME amewataka kila mmoja kujiuliza kama eneo lake analoliongoza au kama kiongozi wa familia je eneolake linausalama wa kutosha? Je sio eneo ambalo wahalifu wanaweza kuligeuza kuwa maficho ya kuandalia mikakati ya kutekeleza matendo yao ya kiuhalifu?
Pia aliwaeleza kuwa ni jukumu lao kama viongozi kuwaeleza wanaowaongoza wajihadhari na kutoa taarifa wanapoona wanapoona wenyenia ovu wanapotumia kivuli cha dini kufundisha na kueneza itikadi kali na vitende ambavyo vinaweza kuleta matukio ya kigaidi.
Alisisitiza wawaelimishe wananchi wao kutoa taarifa wanapoona watu wanaobadili malengo mema ya kuanzisha nyumba za ibada na kuzigeuza kuwa nyumba za kufundishia judo na karate na kuficha wahalifu.
Nae Shekhe Ahmad Said kwa niaba ya Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma katika mkutano huo amesema bila ya kuwa na amani hatuwezi kufanya ibada katika nyumba za ibada wala kusoma katika madrasa, shule wala vyuo vikuu kwani uislamu toka ulivyoanza unahubiri amani, umoja, uvumilivu, mshikamano, utulivu na kuheshimiana hivyo mtu mmoja atakayekwenda kinyume na maagano hayo atakuwa ni yeyebinafsi na sio uislamu wala mafundisho ya dini.
Pia Shekhe Ahmad Saidamesema yeye kama kiongozi wa dini yupo tayari kuwafichua watuwasiotaka kufuata sheria nahata kama kunamsikiti unaohatarisha amani na utulivu ili kuepusha matukio yanayoweza kutokea kama yaliyotokea nchi jirani.
Vilevile Katibu Mkuu Jimbo kuu la Dodoma Padre Thomas V. Lali amesema kuwa vitabu vyote vya dini vinasisitiza amani na utulivu. Hivyo hatuwezi kushughulikia amani na nje ya nafsi zetu wakati ndani ya nafsi zetu hatuna amani.
Amesema elimu hii iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma katika mkutano huo iwe endelevu kwani watu wengi hawana elimu hiyo hivyo hivyo amewaomba viongozi kusambaza elimu hiyi ili kumaliza matishio ya ugaidi nchini kwetu tuweze kuishi kwa amani na utulivu.
Aidha Mwenyekiti wa balaza la wazee Mkoa wa Dodoma Balozi mstaafu Job Lusinde amesema tunapaswa kuitunza amani kwani bila amani hakuna maendeleo katika nchi yeyote ile.
Amesema kiongozi anapaswa kuwa mzalendo na nchi yake vivyo anapaswa kushirikiana na wanachi kufichua uhalifu mapema kabla uhalifu haujatokea, pia kiongozi anapaswa kuwa mtunza siri ili kuwepo ushirikianao baina ya vyombo vya dola na wananchi.
No comments:
Post a Comment